
Wadau wa Manchester, UK, wamejiandaa kusherehekea Uhuru wa Tanzania na Kenya Ijumaa tarehe 11/12/09 kwenye ukumbi wa Alter Ego ambayo iko hapa hapa Manchester.
Tiketi za hii sherehe sasa zinauzwa kwa £7.00 lakini pale mlangoni ticket zitauzwa kwa £10.00.
Sherehe itaanza saa 4 usiku ambapo chakula cha Kitanzania kitapikwa na kuuzwa kwa £5.00 kila sahani mpaka saa 6 za usiku na baada ya hapo take-away zitakuwepo kwa bei zaidi.
Ma-DJ kwa siku hiyo ni kama ifwatavyo:
★ DJ COLLO ( bongo flava,genge,kwaito,afro beatz )
★ DJ QUEST ( r n b,hip hop, mtalaamu wa bashment )
★ DJ MORRIS ( mtalaamu wa afro beatz )
TIKETI ZINAPATIKA KWA:
SHARIFF MOHAMMED: 07988356791
KARIBUNI SANA.....................

Golikipa wa timu ya Uganda Revenue Authority, Kaweesa Eddie akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa kimataifa dhidi ya TRA wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Tanzania ilishinda 1-0.

Meneja masoko wa bia ya kilimanjaro, George Kavishe akizungumza wakati wa uzinduzi wa tangazo la biashara kwa njia ya televisheni lililotengenezwa na kampuni hiyo kupitia kampeni yake ya "Fikisha Tanzania katika hatua ya juu zaidi" uliofanyika jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulifanyika Trinity bar, Oysterbay, jijini Dar
Kaka Michuzi
Pole sana na kazi yako nzito yakutupa taarifa mbalimbali zinazotokea ulimwenguni na hasa nchini kwetu Tanzania.Kwa niaba ya TASABA chama cha wanafunzi watanzania waishio Bangalore India ninakuomba ututangazie blog yetu hii mpya ya:
TASABA.BLOGSPOT.COM
kwenye blog yako ili tuweze kuwafikia watanzania wenzetu mbalimbali wakiwemo wazazi,serikali na jamii nzima kwa ujumla ili waweze kupata taarifa ya mambo mbalimbali yanayoendelea India.Kufanikiwa kwa jambo hili itasaidia jumuiya hii kupiga hatua kubwa sana.
wako mtiifu
TASABA spokesman
Jumanne R Mtambalike

Profesa Ali Mazrui, akiwasilisha mada kuhusu masuala mbali mbali ya kijamii na kitamaduni ambayo nchi za Bonde la Nile (Nile Basin Countries), zinavyohusiana hususan katika suala zima la rasilimali za maji na matumizi yake wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya Ushirikiano wa nchi hizo, Dar es Salaam juzi. Kulia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya.