FotoBaraza.Net

Young

FOTOBARAZA FOUNDATION

Maelezo

FOTOBARAZA FOUNDATION

Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.Huu ni mfuko wa kuchangia kimawazo na chochote kitu kwa watanzania wote wenye kuhitaji msaada wetu wa hali na mali kama vile yatima,maalbino,wanawake wenye matatizo,wazee,vilema na kusaidia jamii yote kwa ujumla.

Wadau: 79
Latest Activity: Dec. 10, 2009

Uwanja wa Mijadala

Young

Wadau wa UK kukutana kupeleka mbele gurudumu la Fotobaraza Foundation 1 Reply

Umeanzishwa na Young. Mchango wa mwisho na Mama Malaika Dec. 10, 2009.

Babukadja

TAARIFA FUPI YA KIKAO CHA TATU 8 Replies

Umeanzishwa na Babukadja. Mchango wa mwisho na Oswald Jonh Akyoo Jun. 11, 2009.

john mwakyusa

MAONESHO YA PICHA ZA YATIMA WETU 4 Replies

Umeanzishwa na john mwakyusa. Mchango wa mwisho na Maingu Jan. 27, 2009.

Ukuta wa Maoni

Weka Maoni

Lazima Uwe Mdau wa FOTOBARAZA FOUNDATION ili Kuweka Maoni

alma Maoni na alma saa Agosti 14, 2008 4:02pm
**natamani kuwaona na kuwajua wanakijiji wenzangu tupate kupeana mawazo tofauti katika maisha**
umoja ni nguvu
Mkwaya Maoni na Mkwaya saa Agosti 14, 2008 10:11am
Hayahayahaya mkutano wa utakuwa siku ya jumamosi tarehe 16 pale makumbusho saa nane mchana. karibuni wooote
EDO NDAKI Maoni na EDO NDAKI saa Agosti 11, 2008 3:26pm
Pongezi kwa wale woote walioshiriki kwa namna moja au nyingine.Pia pongezi kwa wale wote mliotoa maoni au kama umesoma lakini hukutoa,pia mchango wako ni mkubwa.


Maoni yangu:

Kwanza lazima katiba yetu, ibainishe kutakuwa na mikutano au mkutano mkuu mara ngapi katika kipindi cha mwaka mmoja.Tunaweza kukubalina baada ya miezi mitatu au mara mbili kwa mwaka au mara moja kwa mwaka.Mikutano mikuu inakuwa na lengo la kuangali kwa undani mwelekeo wa kikundi na unakuwa na uwezo wa kufanya marekebisho ya baadhi ya vifungo vya katiba iwapo zaidi ya asilimia 50 ya wajumbe wa wanaopaswa kuwepo kwenye kikao kuhudhuria.Pia kupitia taarifa ya utendaji ya kikundi kutoka kwa katibu na fedha kutoka kwa mweka hazina.

Ikumbukwe mkutano mkuu hauzuii kuwa na mikutano ya kila mwezi mliyopendekeza au haipingani na kuwepo na mikutano ya dharurala inapobidi.

Bado wanakikundi nahitaji kuangali kesho zaidi ya leo ninapoandika maoni yangu.

Katiba imeonyesha majukumu ya viongozi.Safi sana.Ila itapendeza kuweka bayana,viongozi wanatakuwa wanapatikana vipi?kuchanguliwa?kuteuliwa? Na je watakuwepo kwenye madaraka kwa muda wa siku,miezi au miaka,miongo mingapi(ka utani kidogo ili usichoke kusoma..aa)Hivyo katiba ionyeshe japo kiongozi atakuwepo madarakani kwa muda gani.

5.1 KIKUNDI KUFILISIKA
i. Lengo kuu ni kuwa na maendeleo mazuri ya kikundi ya jitihada zake za kule watoto yatima, hivyo jitihada za makusudi zifanyike ili kikundi kidumu

Kuhusu kufilisika kwa kikundi.Hapo lengo la hilo neno ni zaidi ya linavyosomeka.Kufilisika au kufika kikomo kwa kikundi lazima kuweke bayana ingawa siyo malengo yetu.Kikubwa mamlaka zinapenda kujua vikundi vinavyojishughulisha na masuala ya pesa mwisho wa siku mali za kikundi zitaenda wapi?

Mfano:-Kikundi kikawa "laptop",pesa zaidi ya milioni mbili benki na samani zingine.Inatokea mamlaka (serikali)wanatupiga marufuku kuendelea na shughuli zetu kwa sababu moja ama nyingine.

Hapo ndio umuhimu wa kipengele hicho unapokuja. LAZIMA kikundi kiweke baya mfano:-Kikundi kikifilisika au kufika kikomo,Mali za mfuko wa Yatima wetu zitagawanya kwenye kituo/vituo vya kulelea watoto ambavyo wajumbe watapendekeza.

Hii itawapa moyo wafadhili kuona iwapo ikitokea mwisho(mungu tuepushie)lakini bado tutamaliza kwa kufanya jambo la kijamii bila faida binafsi.

Asanteni sana kwa kusoma maoni yangu.
Nitakuwa nanyi hiyo agust 16 kwa njia ya simu ya kiganjani ..kufafanua au kuchangi zaidi.

Kazi nzuri inawezekana
Mama Malaika Maoni na Mama Malaika saa Agosti 9, 2008 1:50pm
Asante na karibu sana Father Kidevu
Father Kidevu Maoni na Father Kidevu saa Agosti 5, 2008 9:25am
Jamii ya humu ndani nawasilimu sana sana na tupo pamoja kwa kila jambo.
Mkwaya Maoni na Mkwaya saa Agosti 5, 2008 8:52am
Mambo yanaendelea kupamba moto, tunakaribia kuweka maneno kuwa matendo, Karibu Clarrisa na wageni wengine wote.. pamoja tutafika
Mkwaya Maoni na Mkwaya saa Julai 30, 2008 11:43am
wadau Katiba ndo ishatuaa kijijini tafadhali muisome tuanze safari yetu kwa amani upendo na mshikamano
Maingu Maoni na Maingu saa Julai 28, 2008 12:48pm
haya viongozi tupeni ratiba ya vikao,na nini kinajiri punde.
maana tuna njaa nacho hicho kikao mpaka tunakaribia kupata vidonda vya tumbo.
pamoja sana tuu.
Federal Agent Maoni na Federal Agent saa Julai 26, 2008 11:10pm
Aise hii ni aibu niko dar alaf sijahudhuria kikao, ingekuwa hata ni nafasi nzuri ya kuwafahamu wadau.
Nijulisheni kikao kingine ni lini ili na mimi nitie maguu.
EDO NDAKI Maoni na EDO NDAKI saa Julai 25, 2008 11:35am
amina RT na Mkwaya kwa kutambua kamchango kangu.

kikao kijacho naomba katibu japo nistue na mimi japo nichangie kwa kutwanga ka simu...aaa aaa

siku njema wangu
 

Wadau (79)

Young Michuzi Jr EDO NDAKI Mama Malaika Mkwaya Bonny Babukadja Maingu mujydebubyz Don Magere john mwakyusa Ritha T Meshack maganga Alfan araway Evacindy Bigambo milya Father Kidevu komredi KITOJO ANGEL NEHEMIAH Rugambwa james jingo Lucky Ekonjo ringomoses Helen Mipawa Cat Wa Ukweli. ANJELA
 
 

Besdei za Kuzaliwa

 

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter