MUHTASARI WA MKUTANO MKUU WA TATU WA KIKUNDI CHA YATIMA WETU – FOTOBARAZA KILICHOFANYIKA TAREHE 16/08/2008 KATIKA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO – KIJITONYAMA.
1.0 WALIOHUDHURIA
2 Angel Nehemiah Mwenyekiti
3 David Ekonjo Makamu Mwenyekiti
4 Neema Mkwaya Makongo Katibu
5 Othuman Michuzi Katibu Msaidizi
6 Ritha Tabaro Mtunza Hazina
7 Philemon Msangi Mlezi
8 Chaoga Tonge Mjumbe
9 John Mwakyusa Mjumbe
10 Emanuel Maingu Mjumbe
11. Luihamu Ringo Mjumbe
1.2 AGENDA NA 1. KUFUNGUA KIKAO
Mwenyekiti alifungua kikao mnamo saa kumi kamili (16:00) jioni kwa kumshukuru Mungu kuweza kutukutanisha na kuwakumbusha wajumbe washiriki kikamilifu katika kuchangia mawazo yao kwa umakini na uwazi.
1.3 AGENDA NA. 2 KUPEANA MLISHONYUMA WA MAJUKUMU ALIYOTOLEWA KIKAO KILICHOPITA
Nembo,
Kikao kilichopita awajumbe walipendekeza kuwepo na nembo ya kikundi, hivyo ikaagizwa kila mwanakikundi atakayeweza kupata awasiliane na Maingu, Bwana Ekonjo alifanikiwa kuipata, akaiweka barazani kwa ajili ya maoni, na imeonekana kuwa kati ya zile tatu nembo namba tatu itafaa ila itafanyiwa marekebisho madogo.
Muhuri na kitabu cha stakabadhi:
Jukumu hili alipatiwa Babkadja, amefanikiwa kutengeneza muhuri ambao aliwasilisha kwa wanakikundi, ukaonekana unafaa hivyo umepitishwa.
Kuhusu kitabu cha stakabadhi, imeonekana ni vyema ikasubiriwa nembo na namba ya utambuulisho ya mlipa kodi (TIN), hivyo baada aya kupatikana hivi kitabu kitakuwa tayari.
Fomu za kufungua akaunti ya benki
Fomu za bank ya Barclays zilipatikana. Fomu hizi zilihataji kujazwa na watu watatu kutoka kwenye kikundi, hivyo ilikubaliwa kuwa ijazwe na Mwenyekiti, Katibu na Muweka hazina.
1.4 AGENDA NA. 3 KUPITIA NA KUJAZA FORM ZA KUJIANDIKISHA
Mwenyekiti akishirikiana na wajumbe wengine waliweza kupitia na kujaza fomu ya kuandikisha kikundi.
Mambo Muhimu
• Pesa taslimu shillingi laki moja na nusu zilihitajika kwa ajili ya kujiandikisha, ambapo sh 10000 ni kwa ajili ya fomu, shilingi 40000, ni ada ya mwaka na sh 100000 kwa ajili ya .................., fedha hizi zilipatikana siku hiyohiyo baada ya wajumbe kuchanga na kupatikana kiasi cha shilingi laki moja, pamoja na zile zilizochangwa kikao cha pili zilifika shilingi laki moja na hamsini(150000)
• Zilihitajika barua kutoka kwa wizara husika......
Mengineyo;
Mjumbe Edo alipiga simu na kuchangia kwenye marekebisho ya katiba, alichangia kuwa kiongezwe kipengele kitakachoonyesha, ikitokea kikundi kimefilisika mgawanyo wa mali au samani lazima uwekwe bayana,
Ilikubaliwa kuwa kundi likiflisika au likifikia ukomo au kufutwa na serikali, basi thamani na fedha zote zitagawiwa kwa kundi la watoto yatima watakao pendeekezwa na kamati kuu ( kikundi kilichokuwa kinafuata kutembelewa/ kupewa masaada)
Tags:
Shirikisha
-
▶ Jibu Hoja Hii