FotoBaraza.Net

Michuzi Jr

MUHTASARI WA MKUTANO MKUU WA TANO WA KIKUNDI CHA YATIMA WETU – FOTOBARAZA KILICHOFANYIKA TAREHE 25/10/2008 KATIKA UKUMBI WA CHAGA BITE – KIJITONYAMA DAR ES SALAAM

1.0 WALIOHUDHURIA
1. Angel Nehemiah - Mwenyekiti
2. David Ekonjo - Makamu Mwenyekiti
3. Othman Michuzi - Makamu Katibu
4. Ritha Tabaro - Mtunza Hazina
5. Sadick Kalula - Mjumbe
6. Edo Ndaki - Mjumbe (kwa njia ya simu)

1.2 AGENDA NA 1 KUFUNGUA KIKAO
Mwenyekiti alifungua kikao mnamo saa kumi na moja kamili (11:00) jioni kwa kumshukuru Mungu kuweza kutukutanisha tena katika kujadiliana machache..

AGENDA NA. 2 REPORT JUU YA MAENDELEO YA USAJILI WA YATIMA WETU – FOTOBARAZA
(A) Kutokana na kuwa jukumu zima la usajili lilikuwa mikononi mwa M/Mwenyekiti wajumbe wote walikuwa tayari kupokea report/maendeleo ya usajili ulipofikia. Alisema kuwa kule Wizara ya mambo ya ndani walimuahidi kuwa usajili ungekuwa tayari kufikia tarehe 15/10/2008 lakini kwa bahati mbaya siku hiyo jina Letu halikutoka,na kutokana kuwa na majukumu ya kikazi,M/Mwenyekiti alishindwa kufuatilia ni kwa nini jina letu halikutoka kwa siku hiyo sababu alikuwa safarini Geita kikazi. Lakini hata hivyo kuna mtu wa pale Wizarani alijaribu kuwasiliana nae akiwa kule kule Geita kutaka kujua ni kwa nini jina letu halikutoka siku ile lakini kwa bahati mbaya na yule mhusika alikuwa safarini Bukoba na kumuahidi kuwa angekuwa amerudi situ ya jumanne tarehe 29/10/2008. Kwa sababu M/mwenyekiti naye alipanga kurudi Dar es Salaam basi walikubaliana kuonana pale Wizarani siku hiyo ya jumanne kwa ufuatiliaji zaidi.

Baada ya ripoti hiyo M/mwenyekiti aliomba usaidizi katika ufuatiliaji wa swala hilo zima la usajili kwani majukumu yalikuwa mengi sana kwa upande wake na mbaya zaidi alitakiwa kurudi tena Geita siku ya alhamisi. Alipendekeza wasaidiane na Othman Michuzi (jr) kwani inaweza kuwa rahisi kwake kwa sababu yuko maeneo ya mjini kikazi.

Kwa bahati nzuri Michuzi jr nae alikubali majukumu hayo ya ufuatiliaji wa usajili lakini naye pia alipendekeza kwa kipindi ambacho M/mwenyekiti hatokuwepo basi wasaidiane na Mjumbe mwingine ambaye ni Ndugu Emmanuel Maingu katika ufuataliaji huo. Wajumbe wote walikubaliana na mawazo hayo.

AGENDA NA 3. RIPOTI YA FEDHA (MICHANGO)
Mwenyekiti alimuuliza Mtunza hazina kama mpaka sasa kuna michango yeyote aliyoipokea, naye alisema mfuko una Tshs. 55,000. Baada ya taarifa hiyo M/mwenyekiti David Ekonjo na Mjumbe Sadick Kalula walitoa Tshs. 10,000/= kila mmoja kama sehemu ya kuendelea kutunisha mfuko wa YATIMA WETU – FOTOBARAZA. Kutokana na michango hiyo mpaka sasa mfuko wetu una jumla ya Tshs. 75,000/=

MENGINEYO:
Mtunza hazina alipendekeza kuanza kutembelea vituo vya Watoto Yatima kama itawezekana kwani siku zinazidi kwenda bila kulitekeleza lile tulilolikusudia. M/mwenyekiti alichangia kuwa ni vizuri tukasubiri usajili ukamilike tu kwani kwa kufanya hivyo inaweza kuleta shida badea na kukosa utetezi wowote kwani kikundi bado hakijapata kibali rasmi cha kufanya lolote. Wajumbe wote walikubaliana kusubiri hatma ya usajili kwani mambo mazuri daima hayataki haraka. Mwenyekiti alisisitiza kuwa ofisi ya Mtunza hazina iko wazi wakati wote kwa hiyo mwenye chochote asisite kutoa. Mwenyekiti alizidi kuwaomba wana YATIMA WETU – FOTOBARAZA wasikate tamaa kwani mpaka sasa matumaini bado yapo ya kupata usajili isipokuwa kama tujuavyo mambo ya Serikali yetu yalivyo.

MWISHO:
Mwenyekiti alifunga kikao saa moja kamili (1:00) jioni kwa kumkabidhi Mungu ili akiimarishe kikundi katika utekelezaji wa msimamo wa Dira ya kikundi kwa maendeleo ya Watoto Yatima kwa ujumla wake.

………………….
MWENYEKITI

Shirikisha Twitter

Jibu Hoja Hii

Michango ya Mjadala Huu

Hongereni sana kwa kukutana na kufanikisha hatua KUBWA nyingine.
Safari naamini inaendelea vema na ninaamini tutafika TU.

KILA LA KHERI UMOJA NI NGUVU

Jibu Hoja Hii

pamoja kaka EDO.

Jibu Hoja Hii

pamoja daima

Jibu Hoja Hii

RSS

Besdei za Kuzaliwa

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter