WAZO TU
KWA KUWA
Sisi tuliowanachama wa yatima fotobaraza tunaunganishwa na vitu vikuu vine
1.Mapenzi yetu ya lugha adhimu ya Kiswahili
2.Mapenzi yetu ya sanaa ya picha
3.Moyo wetu wa kusaidia yatima walioko katika jamii yetu
4.Mapenzi yetu ya kupenda kusocialize(mkwaya nisaidie tafsiri yake ya Kiswahili)
BASI:
Tuelekeze lensi za kamera zetu kuchukua matukio , mazingira wanamoishi watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi. Halafu siku moja kuwe na maonesho ya picha kwa jamii katika moja ya hoteli hapa Dar- lengo kuhamasisha jamii kuhusu janga hili, na pia kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza huduma zetu hizi.
ISIYO MUHIMU
Naadika wazo hili kutokea hapa millennium tower. Nilipopita karibu na sehemu yetu tunaposocialize ndipo wazo likanijia . nikaingia hapa na kuanza kuandika kabla sijapata msongo mbadala wa maisha.
PAMOJA
NI MIMI MWANA YATIMA WETU FOTOBARAZA
JPM
NK. NAKARIBISHA MAONI ,MAWAZO , MABORESHO
Tags:
Shirikisha
-
▶ Jibu Hoja Hii