E bwana Chaoga kwanza nikupongeze kwa ujasiri wako na uelewa ,maana ktk kipindi hiki ambacho waTanzania wanamponda jamaa wewe umesimama kidete kumtetea! Kwa kifupi tunahitaji wazalendo kama wewe. Unajua kama kuna viongozi bogus duniani basi ni Bush na Blair lakini katu huwezi kusikia Mmarekani au Muingereza anamtukana hadharani kiongozi wa nchi but wanakua na ukosoaji wenye kujenga kwani wanaelewa kuwa raisi siyo mtu bali ni cheo cha ukuu wa nchi, so kumtukana raisi ni sawa na ndege Kurumbizi anayetukana kichaka alichokalia. Watanzania wengi badala ya kutoa ushauri wanchukua chuki binafsi na kushabikia habari za magazetini bila kufanya upembuzi yakinifu (Hapa sasa sijui tatizo ni elimu au la!) wanasahau kuwa hata waandishi wa magazeti wana itikadi na ajenda zao za kisiasa, mfano angalia hadithi ya kurushiwa mawe raisi jinsi jinsi ilivyoripotiwa tofauti. Mimi ushauri wangu ni kuwa tumuunge mkono raisi katika yale mazuri afanyayo na yale mabaya basi tutoe ushauri chanya maana yeye sio Mungu lazima atakosea(Hata Mwalimu alisema hili ! tuyaache yale ya kipumbavu tuyafuate mema). Kwa mfano mimi sikubaliani na sera yake ya kusema kamwe Tanzania haiitaji uchumi wa dola maana ni ukweli usiofichika kuwa hakuna kamwe duniani ubepari (Capitalism) wa asilimia 100 na hata hao wakuu wanaotuambia tuwe na free market economies dola zao zinadhiti maeneo nyeti ya uchumi. Kwa hiyo nashauri japo ubepari hauzuiliki but tujaribu kuweka safety nets japo katika sehemu nyeti. Mfano suala la mikataba ya madini,financial markets (Interest and exchange rates) na soko la ajira serikali lazima iweke meno yake tusiwaachie mabepari watukalie kwa kigezo wawekezaji. Mwisho nampa big up JK kwa msimamo wa nchi kuhusu East African Community,utawala wa kisheria na busara na uvumilivu mkubwa nimemini yeye ni mpiganaji. Ni hayo tu kwa leo mkuu!
Sishangai Alfan wabongo wengi hata mimi ni wavivu wa kusoma!( But sio kusoma kiu na uwazi) na hapo ndipo wenzetu wanapotupiga three points za kumwaga halafu tunamlalamikia JK! Teh,teh,teh,teeeeeeeeehhhhh. Ni hayo tuuuu!
nashukuru MCHUNGAJI kwa maelezo yako wengi watakuwa wamekupata sema tu sisi wabongo ndio tulivyo ni rahisi sana kuukubali uongo kuliko ukweli!!! na huwa hatupendi kutoa sifa stahili kwa mtu aliefanya kizuri sie kazi yetu ni kusubiri afanye vibaya ndio tuseme!!!
lete sababu neema usumuhukumu mtu bila kumuelezea kosa lake ili alielewe, isije ukaleta sababu binafsi kumchukia mtu, kumbuka uraisi ni cheo cha juu kabisa cha nchi sasa isije ikawa umeudhiwa na mjumbe wa nyumba kumikumi ukamchukia KIKWETE...!!