FotoBaraza.Net

Bby Candy

PIGA VITA MAUAJI YA ALBINO

Maelezo

PIGA VITA MAUAJI YA ALBINO

HALI INATISHA KWA NDUGU ZETU WENYE ULEM AVU WA NGOZI, WAMEKUWA WANAWINDWA KAMA WANYAMA. EBU FIKIRIA NDUGU MWANAKI JIJI KIFANYIKE NINI KUWAKOMBOA DADA ZETU, KAKA ZETU,WADOGO ZETU NA HATA WAZAZI WETU MAALBINO ILI WAEPUKANE NA JANGA HILI.

Wadau: 12
Latest Activity: Jun 6

Uwanja wa Mijadala

Anzisha Mjadala

Nobody has added any discussions yet! Add a discussion to get started.

Anzisha Mjadala

Ukuta wa Maoni

Weka Maoni

Lazima Uwe Mdau wa PIGA VITA MAUAJI YA ALBINO ili Kuweka Maoni

Alfan Maoni na Alfan saa Januari 28, 2009 10:38am
Hahahhahahaha! Candy umenifurahisha sana japo natakiwa kuhuzunika kutokana na mauaji haya ya ndugu zetu!Nimecheka kwa sababu nahisi nawe unaogopa wanaweza kudhani ni albino wakakugeuza deal! hahahhaaaha! Just joking my dear, usikasirike! Tuko pamojah katika kupinga na kukomesha mauaji ya ndugu zetu hawa!
E.B.M Maoni na E.B.M saa Januari 19, 2009 10:53am
jamani ndugu zetu wa KAGERA mnaenda wapi? mmeua tena albino mwingine tena?????
E.B.M Maoni na E.B.M saa Januari 17, 2009 3:44pm
today ihave been very disappointed after getting news that another Albino ameuwawa kwa kukatwa miguu na mikono huko kagera .
CHA the Great Maoni na CHA the Great saa Januari 17, 2009 3:18pm
VIZURI SANA DADA KWA KUANZISHA HII KITU..NA MIMI KAMA MWANAPAMOJAH MWENZAKO, NAUNGANA NA WEWE KULAANI MAUAJI DHIDI YA NDUGU HAWA. SIUNGANI NA WEWE KATIKA GROUP YAKO KWA KUWA WEWE NI MWANA "PAMOJAH", BALI NAUNGANA NA WEWE KWA SABABU HALI HII INAMHUSU KILA MTU ALIYE NA UPENDO NA HURUMA NA BINADAMU MWENZAKO, KWA KWELI NCHI YETU IMEKUWA NA ALAMA MBAYA SANA KUTOKANA NA HAYA MAUAJI YANAYOENDELEA. HAYO NI MACHACHE TU. MENGINE NITAKUJA KUCHANGIA NEXT TIME.

PAMOJAH WE CAN STOP MAUAJI DHIDI YA ALBINO
Ekonjo Maoni na Ekonjo saa Januari 15, 2009 8:54am
Hii inatisha kwa namna zote, kuanzia ndugu,wazazi,walezi wa hawa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi, hivi kweli kama inafika hatua kwamba unamuuza ndugu yako kisa pesa (mambo ya kuuzwa kwa Yusufu hao , kwa wale wasomao vitabu vya dini) na kwa wale wanaovamiwa na kuuwa au kukatwa viungo, Swali ni Je kuna uwekano kwamba ndugu wanahusika moja kwa moja kutengeneza mchongo ili uvamizi ufanyike? na kisha kujifanya kwamba wamevamiwa?

Kila kitu kinawezekana, Je hawa ndugu zetu (Albino) wakiamua kuwa vibaka , au waporaji simu na vitu vidogo , Je utathubutu kumkimbiza au kumwitia mwizi? Sidhani kama Kuna kiumbe atakuelewa?
Nini Kifanyike?
(i) Marufuku waganga
(ii) Makambi ya Albino
(iii) Jamii kuelishwa juu ya Imani Potofu?

Toa mchango wako, inawekana kwa namna moja au nyingine tukasaidia kutokomeza Hili.
Maingu Maoni na Maingu saa Januari 15, 2009 8:25am
Hii hali ni mbaya mno.
Haipaswi kuachwa bila kuikemea.
Swali la kujiuliza hapa ni Je,Ungekuwa wewe/mimi ndio mlemavu ama hata mwanao ungesadiki kumtoa kafara ili upate mali,na ukisha pata unazitumia na nani???
cherry Maoni na cherry saa Januari 15, 2009 2:15am
Sadiki unavyo sema nahisi ni kweli kua mauaji haya inawezekana yalianza zamani lkn hayakupata kutangazwa kama siku hizi ila Candy umeuliza swali la kama nishawahi sikia kilio cha albino,ukweli sijawahi najaribu pia fikiria hata kama nishawahi ishi karibu na albino pia sifikirii unajua vile ni rare condition inakua si rahisi kujua hata kama kafa.Kingine napenda kujua kuna yule mbunge wa kike zeruzeru Michuzi hupenda kumuweka sana tu anapo hudhuria bungeni hivi katoa maelezo yoyote juu ya hili tatizo au kaamua kuuchuna maana yeye yupo jikoni kabisa angekua mstari wa mbele kupigania haki ya wenzie.Na pia kuliwahi kua na mjadala hapa fb wa albino nini kifanyike kusaidia nilitoa idea ya watu/vijana wanao ishi karibu na albinos wangejitolea kulala ile staili ya kolokoloni ili kupigana na janga hili,nimeona hii style kwenye documentary ya South Africa,walikua wanauliwa watu kwa ajili ya viungo vyao vya sehemu za siri kwa imani kama hizi za mauaji ya albinos wananchi wakaamua kujipanga kihivyo kwasababu wakisubiri serikali haifanyi kitu ni maneno tu,na wakasema imepunguza mauaji sana tu.
EDO NDAKI Maoni na EDO NDAKI saa Januari 14, 2009 11:10pm
nitakuja kuchangia baadaye ila kikubwa..nakupongea kwa kuanzisha hili kundi..ni muhimu sana kwa muda tulio nao...

tutafika tu
E.B.M Maoni na E.B.M saa Januari 14, 2009 10:14am
Hakuna mtu aliyechagua kuzaliwa kama alivyo,amezaliwa alvyo kwa mapenzi ya mola,hivyo wote wanao jihusisha na mauaji ya Albino iko siku, adhabu yao wataipata hapahapa duniani
cherry Maoni na cherry saa Januari 14, 2009 4:45am
Eti Candy ni kweli mazeruzeru sasa wamepewa simu za mkononi ili wapambane na hili tatizo??
Mie naona kama serikali iko serious kutatua tatizo hili wange sema kua atakae toa maelezo ya nani anae jihusisha na mauaji atapewa chochote lkn sio kuhamasisha watu bila changamoto yoyote.Kwasababu mpaka hili tatizo limetokea ni njaa na watu kuhangaika na maisha wanadanganyika na chochote kile sasa na serikali ingetumia saikolojia hio ktk kuteka akili za watu ambao wanajua nani muhusika lkn hawaoni faida ya kutoa maelezo.
 

Wadau (12)

cherry E.B.M Dismas EDO NDAKI Maingu Ekonjo ed Allawi Alfan Dunda Glory Bby Candy
 
 

Kuhusu

Babukadja Babukadja created this Ning Network.

Besdei za Kuzaliwa

 

© 2009   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter