FotoBaraza.Net

Maelezo

MAPISHI CORNER

Uwanja wa mapishi na aina mbalimbali za chakula. mnakaribishwa wadau kutupa aina mbalimbali ya mapishi na chakula.kumbuka hata mchele mmoja unaweza kuupika ktk aina 50 za mapishi.

Wadau: 48
Latest Activity: 1 day ago

Uwanja wa Mijadala

waswa walter wakhungu

Githeri cha malenge(majungu) 2 Replies

Umeanzishwa na waswa walter wakhungu. Mchango wa mwisho na Mabagala Oct. 9, 2009.

mujydebubyz

UPISHI WA KUKU BILA SHIDA 5 Replies

Umeanzishwa na mujydebubyz. Mchango wa mwisho na Mtoto mzuri Oct. 8, 2009.

mujydebubyz

keki 6 Replies

Umeanzishwa na mujydebubyz. Mchango wa mwisho na cherry Sep. 16, 2009.

Ukuta wa Maoni

Weka Maoni

Lazima Uwe Mdau wa MAPISHI CORNER ili Kuweka Maoni

Mtoto mzuri Maoni na Mtoto mzuri saa Ocktoba 8, 2009 11:35am
mhhhh na nilivyo mvivu kuiingia jikoniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii yaani patanisaidia hapa
Ritha T Maoni na Ritha T saa Ocktoba 2, 2009 12:31pm
asante sana dada samira,
yani hapa ukipata ugali wako wa moto ah unainjoy mwenyewe.
Mama Rayan Maoni na Mama Rayan saa Septemba 27, 2009 3:28pm
naona bora turudi jikoni kidogo leo nimetamani ugali na mchuzi wa samaki wa nazi
mahitaji
1-samaki kiasi upendacho
2 vitunguu maji kiasi
3-nyanya kiasi inategemea na uwingi wa mchuzi
4-vitunguu thom kiasi
5-tui la nazi zito
6-mafuta ya kupikia kiasi
7-pilipili mbuzi mbili au hoho moja
jinsi ya kupika
1-kaanga samaki kama kawaida mweke pembeni
2-kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown
3-tia thom
3-tia nyanya kaanga mpaka ziive
4-mimina tui tia na samaki ikichemka tia pilipili kwa ajili ya harufu usisahau chumvi acha iwe nzitonzito
Kisusi Maoni na Kisusi saa Septemba 24, 2009 8:04am
Jamani wadau mbona kimyaaa, au ndo shibe za biriani na pilau za Eid?
Lucie wa mama Maoni na Lucie wa mama saa Septemba 18, 2009 9:47am
Hahaaa sawa my wi, ila mi nina coca cola kubwa zile za lita sijui utamaliza?
Hahaaa pascal hujui kusoma nn?
Kisusi Maoni na Kisusi saa Septemba 18, 2009 9:02am
Ahsante kwa ushauri Massawe
Ritha T Maoni na Ritha T saa Septemba 18, 2009 6:52am
ASANTE SANA LUCIE,
hapa naona kaka angu atazidi kunenepa tu,ntakua nakutembelea kila siku,nakuja na pepsi zangu mbili.
kenvin massawe Maoni na kenvin massawe saa Septemba 17, 2009 7:42pm
wee dct Stiba,wanaume wanaoingia jikoni....mmmmm!! kutakuwa na tatizo mkuu! raha ya mume ni kupikiwa! ukimzohesha mamaaa!!! kuingia jikoni!! hooooo!!!!!! kuna siku atakuja baba mkwe wake!! ujikute ni zamu yako ya kupika!! na siku hy ndy itakula kwako!!!! wewe jichanganye jikoni tu.....ipo siku!
Mabagala Maoni na Mabagala saa Septemba 17, 2009 4:59pm
Hii Zanzibari Pizza naona!mpaka maji ya madafu???
Lucie wa mama Maoni na Lucie wa mama saa Septemba 17, 2009 4:38pm
PIZZA
Vipimo;
Unga 4 Vikombe
Maziwa ya unga 2 vijiko vya supu
Mafuta ya zaituni ½ kikombe
Hamira 1 kijiko cha supu
Chumvi kiasi
Sukari 1 kijiko cha chai
Maji dafu dafu 2 kikombe


NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA UNGA
1. Changanya vitu vyote katika bakuli na ukande unga.
2. Ufunike na uache uumuke.

SOSI YA PIZZA
Kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo 1
Thomu iliyokatwa ndogo ndogo 3 chembe
Sosi ya HP 3 vijiko vya supu
Sosi ya tomato 3 vijiko vya supu
Pilipili manga 1 kijiko cha chai
Oregano ½ kijiko cha chai
Parsley (ukipenda) ½ ukipenda

1. Kaanga vitunguu kisha tia thomu, na vitu vyote iwe sosi.
2. Epua kwenye moto.

Chagua kitu ukipendacho kati ya hivi,
Nyama ya kusaga iliyopikwa
Kuku aliyekaushwa na kukatwa vipande vipande
Sauage zilizokatwa
Salami
Vipande vya nanasi

VITU VYA KUJAZA JUU YA PIZZA
Nyanya zilizokatwa vipande vipande
Pilipili mboga iliyokatwa ndogo ndogo
Zaituni ikiwa za kijani au nyeusi
Cheese ya Mazorella
1. Fanya madonge madogo madogo kisha usukume kidogo tu size uipendayo
2. Paka sosi juu ya unga
3. Tia kiteo upendacho
4. Mwagia vitu vya kujaza juu ya pizza
5. Mwagia cheese
6. Pika katika oveni kwa muda dakika 20 au zaidi hadi ziwive.
Hapo sasa hatukaibishani mwanawane, manake dah
 

Wadau (48)

Kisusi mujydebubyz Mabagala Ritha T cherry Waridipolejeusi Mama Rayan waswa walter wakhungu Majoy mumy Mtoto mzuri EDO NDAKI araway Leila Alfan aloyce Mama Malaika Bonny ed Mm eFrancia Gloriaessy Lucie wa mama Chaoga Tonge Dunda yusam Michuzi Jr www.houseofglamourtz.com Furaha kashinde Nasser M. Nasser
 
 

Besdei za Kuzaliwa

 

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter