FotoBaraza.Net

Maelezo

MAPISHI CORNER

Uwanja wa mapishi na aina mbalimbali za chakula. mnakaribishwa wadau kutupa aina mbalimbali ya mapishi na chakula.kumbuka hata mchele mmoja unaweza kuupika ktk aina 50 za mapishi.

Wadau: 48
Latest Activity: 1 day ago

Uwanja wa Mijadala

waswa walter wakhungu

Githeri cha malenge(majungu) 2 Replies

Umeanzishwa na waswa walter wakhungu. Mchango wa mwisho na Mabagala Oct. 9, 2009.

mujydebubyz

UPISHI WA KUKU BILA SHIDA 5 Replies

Umeanzishwa na mujydebubyz. Mchango wa mwisho na Mtoto mzuri Oct. 8, 2009.

mujydebubyz

keki 6 Replies

Umeanzishwa na mujydebubyz. Mchango wa mwisho na cherry Sep. 16, 2009.

Ukuta wa Maoni

Weka Maoni

Lazima Uwe Mdau wa MAPISHI CORNER ili Kuweka Maoni

araway Maoni na araway saa Desemba 17, 2008 3:27pm
chibiriti hapo mmempa kazi kubwa haswa atoe recipe? minazani atawaambia imepotea! na ED hivyo vi nameless vinapikwaje?
ed Maoni na ed saa Desemba 17, 2008 2:56pm

asusa hizooo!
Ritha T Maoni na Ritha T saa Desemba 17, 2008 10:34am
VADONDE NAKUJIBU SHAIRI LAKO

utapendaje kupika usipende kukata kitunguu,
unaogopa kutoa machozi au kujikata mtu,
na kama umekula kwa nini usioshe vyombo,
huo ni uvivu au una matatizo ya mikono,
na kwa nini usisonge ugali tena kwa jiko mkaa,
maana sio kila siku umeme na gesi vitakua,
na kama umepika lazima usafishe jiko,
la sivyo kale hotelini uwafanyie utakavyo,

hehehehehehe nimelinganisha vina mwanawane
vadonde ntakutafutia kaka angu ye anapenda shughuli zote za jikoni ila tu we mfulie nguo zake.
Ritha T Maoni na Ritha T saa Desemba 17, 2008 10:25am
ASANTE DADA LEILA KWA HILO PISHI...LOL LIMEKWENDA SHULE.CHAKULA KIZITOOO NA KINANUKIA.POLE YAKE VADONDE ASIYEPENDA KUPIKA WALA KUPAKUA.

NA CHIBIRITI UMENTAMANISHA LOL SPAGET HIZO ZINAPENDEZA ZIMEPIKWAJE TUSHIRIKISHE NA SIE.
Leila Maoni na Leila saa Desemba 17, 2008 10:10am
Chibiriti, tupe recipe ya huo msosi plz
CHIBIRITI Maoni na CHIBIRITI saa Desemba 17, 2008 12:08am

Leila Maoni na Leila saa Desemba 16, 2008 4:08pm
Araway, hapa tumia ndizi mshale
araway Maoni na araway saa Desemba 16, 2008 12:35pm
leila hapo umenifikisha dada. nakitamani nikaanze matayarisho mapemaa! lakini kuna ndizi aina nyingi na hapa kwetu tuna kimalaindi, mshale,bukoba na .. sasa sijui ni ndizi gani itakuwa nzuri zaidi kwa mlo huu?

majibu tafadhali.
Leila Maoni na Leila saa Desemba 16, 2008 10:17am
Ndizi Mbichi


VIPIMO

Ndizi mbichi 10
Nyama kilo 1
Nazi 1
Chumvi 1 Kijiko cha chakula
Bizari ya manjano (ukipenda) 1 Kijiko cha chai
Pili pili mbichi 3
Nyanya 2
Kitunguu maji 1
Thomu na Tangawizi ya kusaga 1 Kijiko cha chakula

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Kata nyama vipande vipande na uisafishe.
2. Chemsha nyama weka chumvi, thomu na tangawizi. Iache iwive kisha uiweke pembeni.
3. Kata kata nyanya na kitunguu kisha weka pembeni.
4. Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi.
5. Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria
6. Weka maji kiasi, nyanya na vitunguu ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo.
7. Maji uliyoweka yakikauka mimina supu na nyama ndani ya ndizi.
8. Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda.
9. Weka pembeni zipoe.
10. Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.
ed Maoni na ed saa Desemba 15, 2008 12:19pm
RT uoshaji viombo mimi napenda sasa, si unajua tena waosha vyombo ndio wanaofaidi ukoko na mengineyo hahaha.
 

Wadau (48)

Kisusi mujydebubyz Mabagala Ritha T cherry Waridipolejeusi Mama Rayan waswa walter wakhungu Majoy mumy Mtoto mzuri EDO NDAKI araway Leila Alfan aloyce Mama Malaika Bonny ed Mm eFrancia Gloriaessy Lucie wa mama Chaoga Tonge Dunda yusam Michuzi Jr www.houseofglamourtz.com Furaha kashinde Nasser M. Nasser
 
 

Besdei za Kuzaliwa

 

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter