Jamani mwenzenu naomba mchango wenu. nani abaki nani atoke. kwa kuanzia naona niwaambie; Kwa mawazo yangu Berbatov na Neville wangefunguliwa milango. Kwa neville najua ni ngumu kumfungashia virago kwani amekua na timu tangu utotoni. Kuna mambo mengi yanatucost kwa yeye kushindwa kucope na mchezo sasa hivi. halafu mkumbuke kuwa kuna wakati tunakosa option ya kuziba mapengo mabeki muhimu wanapoumia.
Kingine, mpira sasa hivi ni kasi na control, sawa Berbatov ana control nadhani ya hali ya juu kuliko wachezaji wengi wa ligi kuu. Lakini kasi ni tatizo na iwapo kasi inaanzia nyuma kwenye timu halafu inazimwa mbele, ufungaji utapungua sana. Hasa ukizingatia mfungaji wetu mzuri anaondoka.
hebu leteni mchango, haya i mawazo yangu tu.
Ila tunahitaji watu wenye kasi kama david villa, samuel etoo, na striker mmoja wa russia anaitwa Pavylunichenko - sijui nimekosea jina lake? lakini huyu wa mwisho ana quality kama za Berbatov na ana kasi ya ajabu. fergie anweza kubadili role ya Anderson akawa kiungo mshambuliaji zaidi na kutafuta mtu atakayezia pengo la scholes kwani mzee mzima siku hizi nae naona anaanza kuishiwa. Uliona alivyocheza siku na Barca? Kidogo siku hizi anacheza unnecessary fouls.
Hebu nipeni mawazo hapa
Timu ni nzuri na nina uhakika itachukua ubingwa tena msimu huu.
Tags:
Shirikisha
-
▶ Jibu Hoja Hii