Nilikuwa natoa ombi kwa wadau wote mnaoishi au kusoma UK (England, Wales & Scotland) tupate kukutana weekend moja. Naelewa kuwa wengi wetu tuko busy na kazi, masomo, families, etc. lakini twaweza panga weekend moja tukutane. Sijui mnafikiriaje kuhusu suala hili? Iwapo mnaona ni wazo zuri (YOUNG wakubaliana nami 100%), naomba tuchague sehemu ambayo itakuwa rahisi for transport kwa wote ili tukutane tupate kuonana/kujuana na ikibidi kuongelea kuhusu Yatima Wetu na mambo mengineyo kimaisha, etc.
Hata wale waishio nje ya UK na wanapenda kuhudhuria vilevile wanakaribishwa wote. Chibiriti, Chaoga, Michuzi, Jr, Pascal, etc. mnakaribishwa pia kuwakilisha… LOL…
Mimi niko teyari nitakuja kwa hali na mali na Oswaard kwa kuwa unaniwakilishaga kule Nyumbani sasa hapa nitakuwakilisha lakini naomba haya ipangwe wiki mbili kabla na iwe siku za wiki end ili tuweze kupata nafasi kama itawezekana
MUNGU AKUBARIKI ULIE TOA WAZO HILI AMINI
Nakuunga mkono Mama Malaika, ni vyema wadau wa sehemu za karibu wakawa wanakutana mara kwa mara na kuwakilisha. Natumaini kina Cherry watatuwakilisha huko. Tunawatakia mafanikio mema na msisahau picha.lol.