Nilikuwa natoa ombi kwa wadau wote mnaoishi au kusoma UK (England, Wales & Scotland) tupate kukutana weekend moja. Naelewa kuwa wengi wetu tuko busy na kazi, masomo, families, etc. lakini twaweza panga weekend moja tukutane. Sijui mnafikiriaje kuhusu suala hili? Iwapo mnaona ni wazo zuri (YOUNG wakubaliana nami 100%), naomba tuchague sehemu ambayo itakuwa rahisi for transport kwa wote ili tukutane tupate kuonana/kujuana na ikibidi kuongelea kuhusu Yatima Wetu na mambo mengineyo kimaisha, etc.
Hata wale waishio nje ya UK na wanapenda kuhudhuria vilevile wanakaribishwa wote. Chibiriti, Chaoga, Michuzi, Jr, Pascal, etc. mnakaribishwa pia kuwakilisha… LOL…
ni kweli Oswald... nashukuru kwa kuwa unawakilishwa. Nitapenda kuwepo maoni na mada nyingi tu kuanzia Yatima Wetu, Albino, matatizo ya kina mama, etc. Hivyo mchango wako kimawazo nimuhimu sana.
As long as patakuwa na European beers hamna shida. Ngoja tukusanye nauli nasi tuje tujumuike na wadau wa Ulaya. Ni wazo zuri mama malaika, kama mtafanikiwa kukutana. Magere atakuja na Whisky yake ya kichina anasema inawasha moto!
Mimi ninaunga mkono kwa 150% wazo lako mama Malaika na wadau wa uk tujipange na tukutane kama mama alivyoshauri na sehemu nzuri itategemea na wadau wengi wako upande gani,kwa upande wangu sehemu yoyote itakayopangwa nitakuwepo,wadau wa Uk Tafadhali Dada Cherry pale na wengine wote plz