FotoBaraza.Net

Ni mara kadhaa wanakijiji wa FB tumekuwa tukikutana, iwe ni rasmi au si rasmi, sehemu maalum au kwa kuitana wachache tu, lakini kikubwa ambacho kinaniumiza kichwa na kushindwa kupata majibu sahihi ni hiki:

"NI YAPI MALENGO YA KUKUTANA KWA WANAKIJIJI?"

Tulipokutana SOMA (mahudhurio yalikuwa mazuri sana) tulipanga mambo mengi ya msingi ya kuzungumzia ikiwa ni pamoja na mijadala inayoendelea kijijini lakini pia kubwa mojawapo ikiwa ni utekelezaji wa yale ambayo tunayaanzisha kijijini, mfano "FOTOBARAZA FOUNDATION" na forum ndogondogo zinazojumuika na kufanya kijiji kiwepo. Kiukweli hatujawahi kufanikiwa kutekeleza japo nusu ya hata jambo moja kati ya yale tunayoyakusudia katika mikutano yetu.

Kwa mara ya pili tulikubaliana kukutana Msasani Beach Club kwa ajili ya kujadiliana "live" yale ambayo tunajadiliana kijijini, kwa bahati mbaya mkutano huo haukufanikiwa kuwa na mahudhurio mazuri na mwishowe tukatawanyika bila kutekeleza azma ya mkutano huo.

Wiki iliyopita Tarehe 7/11 wanakijiji wamekutana kwa ajili ya malengo yaliyopangwa lakini mwisho wa siku taarifa tulizozipata ikiwa ni pamoja na picha zilizopandishwa kijijini ziliashiria ya kwamba hakukuwa na jambo lolote la zaidi ya kunywa, kufahamiana na kuongea kisha kutawanyika bila ya kufanya lolote ambalo lingekuwa na muelekeo wa muendelezo wa kijiji chetu katika kufanikisha yale tunayoyakusudia.

FOTOBARAZA ni "Social network" kama ambavyo mwanzilishi Babukadja (Apongezwe) alivyoitambulisha kwetu, nasi wanakijiji tumekuwa humu katika kuendeleza, kukuza na kudumisha "Social network" hii,.

Labda nirudi kwenye swali la msingi; "NI YAPI MALENGO YA KUKUTANA KWA WANAKIJIJI?"

Ntafarijika kuwekwa sawa katika hili; Pascal, Chaoga, Oswald, Cha, Jr, Clara, RT, Dunda, Mama Malaika, Jino Moja, Mathew, Jack, Lucie, Mtoto Mzuri, Babukadja, na wengineo wote ambao ni wanakijiji tafadhalini naombeni sana mfikirie kwa kina na kuweka michango yenu ili tuwe na tija na ufanisi katika kuhakikisha kijiji chetu kinakuwa na manufaa kwetu na jamii nzima kwa ujumla.

Ni Changamoto tu, tupo kijijini kunufaishana na si kubezana na kurudishana nyuma!

Shirikisha Twitter

Jibu Hoja Hii

Michango ya Mjadala Huu

hili nalo NENO!

Jibu Hoja Hii

Nashukuru kwa kulitambua hilo!

Jibu Hoja Hii

Social network ya fotobaraza ilitangaza kwamba kutakuwa na party la wanakijiji,hata mimi, malick na araway ambao tulitoka mbali tulijua tunaenda kwenye party na sio kwenda kujadili mijadala endelevu. Na ndio maana nilibeba chupa ya shampeini ili tuburudike zaidi na wanakijiji. Kama ingekuwa ni kikao cha kawaida, basi mimi na chaoga tungejiburudisha baadae kama ilivyokuwa Msasani siku ile tumekutana. Mara hii kwakweli hatujaalikana kwenda kwenye mijadala.

Ila Dr Stiba swali kwako. Kwanini hukuhudhuria hata kwenye kikao kimoja pekee cha maandalizi? nafikiri haya kama ungeyaongelea pale,a isingekuwa party, ama tungeanza kwa kuweka kikao kwanza halafu ndio tuanze kula party. Pili ambalo naona labda hutapenda kuulizwa ni kwanini hukuja kwa party?

Nawasilisha

Jibu Hoja Hii

Pascal umetoka nje ya "ufunguo", yaani nimekuwekea "beat" ya Kwaya we umeimba Ragga muffin! Jamani wanakiji tuwe tunajibu maswali na si kutengeneza mjadala ndani ya mjadala, mpo wapi kaka Magere na Cha, naona huyu Pascal anahitaji kifimbo cheza!

Jibu Hoja Hii

Mjadala nimeuelewa vizuri, kinachonishangaza ni kwamba wito ulielekezwa mapema na bwana michuzi jr kwamba ni party la wanakijiji? Hivi kwenye party kuna mijadala kweli zaidi ya kusahau shida kwa muda?

Jibu Hoja Hii

Nashukuru kwa mchango wako boss, kacheze cheze maeneo ya nyumbani kwenu wakati unasubiri chakula cha jioni!

Jibu Hoja Hii

Ha ha ha ha ha umenifurahisha sana Stiba kwa kutaja jina la RAGGA MUFFIN, i like that.
Whata gwan man!

Jibu Hoja Hii

Hahahahaaa

Jibu Hoja Hii

Tehee teheeeee teheeeeee, kwi kwiii kwiiiiiiii kwiiiiiii, uuuuwiiiiiii mbavu zangu mie!

Jibu Hoja Hii

Usicheke Dr Stiba, hujanijibu bado

Jibu Hoja Hii

Nikujibu nini tena ndugu yangu! We umeamua kuanzisha mjadala wako ndani ya mjadala wangu, basi subiri kipindi cha ucheshi ulete hoja zako, mi nipo serious na nnachokiuliza hapa!

Jibu Hoja Hii

Hata na mimi nipo serious Dr Stiba. kwnye party there is not time to argue and debate. Wewe ndio unaleta ucheshi. Hata tukipitia mapendekezo ya watu kabla ya sherehe ( na wewe ukiwa mmoja wapo wa wapendekezaji) hukuongelea swala la kukutana na kujadili, na siku wadau wa dar wanakutana kwa ajili ya kujadili party iweje wala hukuhudhuria kabisa. Mambo yameenda kama yalivyopangwa.

Mwenyekiti atafute siku kwa ajili ya debate za mijadala na mapendekezo yote. Nina hakika nitakuja, na hapatakuwa na muda kwa ajili ya kunywa na kufurahi. Lakni siku ile ilipangwa kwa ajili ya party. Naomba usizunguke sana. Jibu hoja zangu, siko kwnye ucheshi

Jibu Hoja Hii

RSS

Besdei za Kuzaliwa

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter