FotoBaraza.Net

Ni mara kadhaa wanakijiji wa FB tumekuwa tukikutana, iwe ni rasmi au si rasmi, sehemu maalum au kwa kuitana wachache tu, lakini kikubwa ambacho kinaniumiza kichwa na kushindwa kupata majibu sahihi ni hiki:

"NI YAPI MALENGO YA KUKUTANA KWA WANAKIJIJI?"

Tulipokutana SOMA (mahudhurio yalikuwa mazuri sana) tulipanga mambo mengi ya msingi ya kuzungumzia ikiwa ni pamoja na mijadala inayoendelea kijijini lakini pia kubwa mojawapo ikiwa ni utekelezaji wa yale ambayo tunayaanzisha kijijini, mfano "FOTOBARAZA FOUNDATION" na forum ndogondogo zinazojumuika na kufanya kijiji kiwepo. Kiukweli hatujawahi kufanikiwa kutekeleza japo nusu ya hata jambo moja kati ya yale tunayoyakusudia katika mikutano yetu.

Kwa mara ya pili tulikubaliana kukutana Msasani Beach Club kwa ajili ya kujadiliana "live" yale ambayo tunajadiliana kijijini, kwa bahati mbaya mkutano huo haukufanikiwa kuwa na mahudhurio mazuri na mwishowe tukatawanyika bila kutekeleza azma ya mkutano huo.

Wiki iliyopita Tarehe 7/11 wanakijiji wamekutana kwa ajili ya malengo yaliyopangwa lakini mwisho wa siku taarifa tulizozipata ikiwa ni pamoja na picha zilizopandishwa kijijini ziliashiria ya kwamba hakukuwa na jambo lolote la zaidi ya kunywa, kufahamiana na kuongea kisha kutawanyika bila ya kufanya lolote ambalo lingekuwa na muelekeo wa muendelezo wa kijiji chetu katika kufanikisha yale tunayoyakusudia.

FOTOBARAZA ni "Social network" kama ambavyo mwanzilishi Babukadja (Apongezwe) alivyoitambulisha kwetu, nasi wanakijiji tumekuwa humu katika kuendeleza, kukuza na kudumisha "Social network" hii,.

Labda nirudi kwenye swali la msingi; "NI YAPI MALENGO YA KUKUTANA KWA WANAKIJIJI?"

Ntafarijika kuwekwa sawa katika hili; Pascal, Chaoga, Oswald, Cha, Jr, Clara, RT, Dunda, Mama Malaika, Jino Moja, Mathew, Jack, Lucie, Mtoto Mzuri, Babukadja, na wengineo wote ambao ni wanakijiji tafadhalini naombeni sana mfikirie kwa kina na kuweka michango yenu ili tuwe na tija na ufanisi katika kuhakikisha kijiji chetu kinakuwa na manufaa kwetu na jamii nzima kwa ujumla.

Ni Changamoto tu, tupo kijijini kunufaishana na si kubezana na kurudishana nyuma!

Shirikisha Twitter

Jibu Hoja Hii

Michango ya Mjadala Huu

Asante sana Dr Stiba kwa mjadala wako kuhusu swali hilo hapo juu.

Ujue hata mimi hadi leo sielewi hatua ipi tumefikia upande wa FOTOBARAZA FOUNDATION..
YOUNG amechangia wazo zuri sana kuhusu mjadala live ili wadau wote wa nje na ndani ya Tanzania tuweze kuchangia na kupendekeza nini kifanyike ili malengo yetu yatimie. FOTOBARAZA FOUNDATION sasa ina mwaka mzima toka ianzishwe. Kwa kufanya hivyo tutafikia ingalau zaidi ya nusu ya malengo yetu hapo FOTOBARAZA FOUNDATION itapotimiza miaka miwili. Ila nawaombeni sana sana wadau wa huko nyumbani mtapokutana tena kwenye kikao kijacho jaribuni kuongelea suala hili la FOTOBARAZA FOUNDATION. Na sie wa hapa UK pia tutaongelea suala hili na tutawapa feedback hapo tutapokutana ingawa bado hatujapanga lini na wapi tukutane.

Shukrani!

Jibu Hoja Hii

Shukriya Mama Malaika, message received and plans are following before we put your advice into implementation! Nisalimie wakwe zangu.

Jibu Hoja Hii

Dr stiba heshima yako mkubwa...hongera sana kwa mjadala huu nadhani it is the time to take actions... But before achievements we need changes and before that we need to know the root of the problem. Unajua kijiji hiki nimekisoma vizuri sana kuna watu wa makundi matatu moja wenye malengo kuendeleza kijiji, hawa ni watu wazuri wa kuwafata na naomba muwe na moyo huo huo msitetereke wala kuvunjika moyo..naweza kuwataja young,mama malaika,dr stiba,jr,rt,majoy,chaoga,maingu"mwanaharakati",babukadja,my husband na mimi mwenyewe kama nimekusahau kukutaja nisamehe ila natumai mchango wako umeonwa na wengi. Pia kuna kundi la pili watu ambao hawajielewielewi na kujitambua uwepo wao hapa kijijini yaani hawa bendera hufata mkumbo huku wapo kule wapo... kama wewe unajijua upo kwa kundi hili naomba ubadilike uwe kama hao niliowataja ...kundi la tatu hili ni la watu vichefuchefu kwa nini nawaita vichefuchefu?hivi wanajamii mnapokubaliana mambo mmoja akaharibu huyo naye uwepo wake unahitajika wa nini?mfano wanakijiji wamechanga pesa kakabidhiwa mtu yeye kaingia nazo mtini au kapewa dhamana ya kitu fulani fatilia hiki kaleta makaratasi makanjanja huyu si kichefuchefu?mwingine anagombanisha watu kijijini kwa maneno yasiyo na kichwa wala miguu mara mtoto mzuri kasema hivi...jr kafanya hivi...rt anatabia chafu...ooo fulani kanipiga marufuku kukuachia komment sababu wewe unamatabia mabaya....mimi binafsi kuna mtu kanidhalilisha sana hapa kijijini siku chache za nyuma lakini nilipomsoma nikajua tatizo lake ... Mtu wa aina hii naye KICHEFUCHEFU....hawa watu hapa kijijini hawafai tena kama mimi ningepewa uongozi wa siku moja ningewafuta kwenye hii ramani ya kijiji....samahanini niliowataja majina nafikisha ujumbe...Back to ur discussion dr miezi michache iliyopita mambo yalikuwa yananyooka pongezi maingu na jr na wanakijiji wote kwa sapoti yao ila walivunjika moyo kwa mambo yaliyotokea....sasa basi ili malengo ya kijiji yatimie inabidi tubadilike na tutakapobadilika natumai malengo yatafikiwa....mimi naona tutafika mbali muhimu umoja,ushirikiano na akili itumike... embu fikiria mtu kama araway,paskal,byanaku chui wanatoka mkoa wanakuja dar na mtu wa kwanza kumuona ni mwanafotobaraza mwenzao chaoga hii ni one step ahead...Chaoga nakupongeza kwa ukarimu wako maana hii minjemba mitatu ilishaanza kusahau makwao....nitarudi tena

Jibu Hoja Hii

Nipo kwenye makundi yote isipokuwa hilo linalokupa kichefuchefu!. Kama ni makubaliano ya kuendeleza kijiji basi siku iyo ni kupanga mikakati na kuona wapi pameteleza.Ila kama ni wakati wa mavuno jamani naomba tusiwe na mijadala. Mimi bado nasimama pale pale.
Sikujua kama kuna watu wana tabia kama izo za kupewa pesa wafuatilie vitu na kuingia mitini bila kufuatilia chochote. Na kweli mwenyekiti na msaidizi wake wako wako wawaadabishe hawa watu? Na huyu wa kugombanisha watu na yeye apewe onyo sio kulalamika pembeni tu. Uhasama haufai kijijini.
Ninao ushuhuda ni kweli fotobaraza imefanya nisahau ndugu waliopo dar. Chaoga ndio mtu wa kwanza kujua safari yangu ya mjini. Halafu baadae ndio ndugu wanafuata.

Jibu Hoja Hii

Nimekupata Mkuu Stiba, lengo la wanakijiji kukutana ni kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu kijiji ili kuona ni namna gani tunaweza kuyatafutia ufumbuzi. Tatizo Watanzania wote tumekuwa wanasiasa, tunaongea sana lakini vitendo hakuna. Kuna mambo mengi sana yamekwishajadiliwa lakini hatujafikia muafaka, sasa naona wakati umefika wa vitendo, na wakati wa blaa blaa uishe ili kuweza kuendeleza na kuimarisha kijiji. Na kijiji hiki kama ambavyo amekuwa akisema Mr. Maingu ni kwamba kinaweza kutoa ajira kwa watu. Kikubwa ni kuwa serious na mambo yetu.


PamoJah

Jibu Hoja Hii

Mtoto mzuri "I Salute u" kuanzia dakika utakayosoma mchango huu umepanda cheo na kuwa "Madam". Hekima na busara zako kila siku zapanda na kuwa za kuleta tija kuliko bla bla! Ahsante sana. Pascal nashukuru sana kwa kurejewa na fahamu na sasa ntakupa jukumu la heshma kwa sababu umenishawishi nikuamini unafaa. The Great nashukuru pia kwa kuliona hilo, tukikutana tutajadili "way forward" kwa sababu mpaka hapa nimeshaona chanzo cha tatizo na tatizo lenyewe. Nasubiri hitimisho la Babukadja na Michuzi Jr nifunge mjadala na kuanza kufanyia kazi mapendekezo ya wanakijiji. Ahsanteni sana.

Jibu Hoja Hii

Mtoto mzuri "I Salute u" kuanzia dakika utakayosoma mchango huu umepanda cheo na kuwa "Madam". Hekima na busara zako kila siku zapanda na kuwa za kuleta tija kuliko bla bla! Ahsante sana. Pascal nashukuru sana kwa kurejewa na fahamu na sasa ntakupa jukumu la heshma kwa sababu umenishawishi nikuamini unafaa. The Great nashukuru pia kwa kuliona hilo, tukikutana tutajadili "way forward" kwa sababu mpaka hapa nimeshaona chanzo cha tatizo na tatizo lenyewe. Nasubiri hitimisho la Babukadja na Michuzi Jr nifunge mjadala na kuanza kufanyia kazi mapendekezo ya wanakijiji. Ahsanteni sana.

Jibu Hoja Hii

Mtoto mzuri "I Salute u" kuanzia dakika utakayosoma mchango huu umepanda cheo na kuwa "Madam". Hekima na busara zako kila siku zapanda na kuwa za kuleta tija kuliko bla bla! Ahsante sana. Pascal nashukuru sana kwa kurejewa na fahamu na sasa ntakupa jukumu la heshma kwa sababu umenishawishi nikuamini unafaa. The Great nashukuru pia kwa kuliona hilo, tukikutana tutajadili "way forward" kwa sababu mpaka hapa nimeshaona chanzo cha tatizo na tatizo lenyewe. Nasubiri hitimisho la Babukadja na Michuzi Jr nifunge mjadala na kuanza kufanyia kazi mapendekezo ya wanakijiji. Ahsanteni sana.

Jibu Hoja Hii

Ndugu Wadau Wapenda,

kwanza kabisa napenda kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Dr Stiba kwa mjadala huu aliouanzisha hapa,maana umekuwa ni mjadala wenye changamoto nyingi sana katika kijiji chetu hiki,Nakushukuru sana Dr Stiba.

Pili napenda pia kutia Shukrani nyingi tena nyingi kwa wale woote waliochangia mjadala huu,kwani bila michango yenu huu mjadala usingefikia hapa ulikofikia sasa. Nawashukuru sana Mabagala,Magere,Mama Malaika,Lucie,Elly,Nsajigwa,Mtoto Mzuri,Cha The Great pamoja na Mkuu Young kwa mchango wenu katika mjadala huu ambao unachangamoto nyingi sana na zenye nia ya kutaka kijiji chetu hiki kuwa Jiji. PamoJah sana wakuu.

Ndugu Wadau Mapenda,

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa kijiji hiki Ndugu Babukadja,napenda kutoa maneno machache juu ya mjadala huu pamoja na kile tunachofikiria kukifanya kwa pamoja kama Ndugu,Jamaa na Marafiki wakuu katika kijiji kimoja.

Najua mjadala huu umekuja kutokana na maelezo yangu niliyoyatoa katika mijadala ya awamu kadhaa zilizopita ambazo sitoweza kuzinukuu hapa maana kila mmoja wetu najua anakumbuka vyema mijadala hiyo,Ni kweli kwamba tumekuwa tukikutana mara nyingi katika kwa kujadili mambo mbali mbali ya kijiji japo mahudhurio huwa yanakuwa hafifu lakini tunamshukuru mungu kuwa mambo huwa yanakwenda.

Katika vikao kadhaa tulivyokuwa tukikaa kwa pamoja kama Wadau wa FotoBaraza,tumekuwa tukijadili maswala mbali mbali yanayoendelea katika kijiji chetu hiki likiwemo lile la FOTOBARAZA FOUNDATION ambalo naweza sema kwamba ndilo lililobeba kijiji chetu hiki.Kiukweli tangu tulipokuwa tumeanza kulihangaikia swala hili ni kweli tungekuwa tumefikia hatua nzuri sana mpaka leo hii.Lakini kutokana na mambo ambayo yalikuwa nje ya uwezo wetu tulishindwa kufikia malengo kiasi ambacho tukajikuta tumekwama sehemu moja bila kufahamu ni nini kitafanyika ili kuweza kusonga mbele.

Kitu ambacho kilitufanya tuanze kujipanga upya (ambapo mpaka sasa tuko katika mpango huo) ili kuweza kuianza upya kabisa safari yetu hiyo tuliyokuwa tukiiwazia kila kukicha ya kuitaka FOTOBARAZA FOUNDATION ifanye kazi yake kama tulivyokuwa tumepanga.

Nimekuwa nikifatilia maoni ya mjadala huu kwa makini sana na kuona jinsi Mabagala na Dr Stiba walivyokuwa wakijibizana na Wadau wengine wakichangia maoni yao kuhusiana na kukutana kwa Wadau siku ya tarehe 07/11/2009 kitu ambacho sikuona kama kingeweza kuleta mjadala mkubwa namna hii.Kitu ambacho ni chamsingi kwa sasa hivi Ndugu Wadau Wapendwa ni kujipanga upya tena vyema kabisa na kusonga mbele moja kwa moja kama yalivyo malengo yetu,Maana kwa kuwa hapo mwanzo tulitereza na kufikia kuanguka kabisa,basi sasa hivi inatakiwa tujipange na tutembee kwa makini katika uterezi huu uliotuangusha hapo awali.

Hivyo Basi tusahau yaliyopita na tugange yaliyo mbele yetu kwa kufanikisha malengo yetu.

naomba Kuwasilisha kwenu hili.

PamoJah Tunaweza.

Jibu Hoja Hii

Kwa heshma na taadhima, nikiwa na akili zangu timamu na bila shinikizo, kwa utashi wangu na maelekezo toka kwa wakuu Michuzi Jr na Babukadja, nachukua nafasi hii kuwashukuruni kwa michango yenu na kuthibitisha ya kwamba: PAMOJAH TUNAWEZA! Nafunga mjadala huu na ndio mwanzo wa mjadala ufuatao.

Jibu Hoja Hii

mie yangu macho tu, ila CHA umenena kuhusu wa TZ siku hizi tumeiga tabia za wanasiasa kabisaa

Jibu Hoja Hii

Kaka Chaoga hakuna wa kutubadilisha ila ni sisi wenyewe ndio tunaweza kujibadili kutoka wanasiasa na kuwa watendaji. Nashukuru kwa mchango wako!

Jibu Hoja Hii

RSS

Besdei za Kuzaliwa

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter