Ni mara kadhaa wanakijiji wa FB tumekuwa tukikutana, iwe ni rasmi au si rasmi, sehemu maalum au kwa kuitana wachache tu, lakini kikubwa ambacho kinaniumiza kichwa na kushindwa kupata majibu sahihi ni hiki:
"NI YAPI MALENGO YA KUKUTANA KWA WANAKIJIJI?"
Tulipokutana SOMA (mahudhurio yalikuwa mazuri sana) tulipanga mambo mengi ya msingi ya kuzungumzia ikiwa ni pamoja na mijadala inayoendelea kijijini lakini pia kubwa mojawapo ikiwa ni utekelezaji wa yale ambayo tunayaanzisha kijijini, mfano "FOTOBARAZA FOUNDATION" na forum ndogondogo zinazojumuika na kufanya kijiji kiwepo. Kiukweli hatujawahi kufanikiwa kutekeleza japo nusu ya hata jambo moja kati ya yale tunayoyakusudia katika mikutano yetu.
Kwa mara ya pili tulikubaliana kukutana Msasani Beach Club kwa ajili ya kujadiliana "live" yale ambayo tunajadiliana kijijini, kwa bahati mbaya mkutano huo haukufanikiwa kuwa na mahudhurio mazuri na mwishowe tukatawanyika bila kutekeleza azma ya mkutano huo.
Wiki iliyopita Tarehe 7/11 wanakijiji wamekutana kwa ajili ya malengo yaliyopangwa lakini mwisho wa siku taarifa tulizozipata ikiwa ni pamoja na picha zilizopandishwa kijijini ziliashiria ya kwamba hakukuwa na jambo lolote la zaidi ya kunywa, kufahamiana na kuongea kisha kutawanyika bila ya kufanya lolote ambalo lingekuwa na muelekeo wa muendelezo wa kijiji chetu katika kufanikisha yale tunayoyakusudia.
FOTOBARAZA ni "Social network" kama ambavyo mwanzilishi Babukadja (Apongezwe) alivyoitambulisha kwetu, nasi wanakijiji tumekuwa humu katika kuendeleza, kukuza na kudumisha "Social network" hii,.
Labda nirudi kwenye swali la msingi; "NI YAPI MALENGO YA KUKUTANA KWA WANAKIJIJI?"
Ntafarijika kuwekwa sawa katika hili; Pascal, Chaoga, Oswald, Cha, Jr, Clara, RT, Dunda, Mama Malaika, Jino Moja, Mathew, Jack, Lucie, Mtoto Mzuri, Babukadja, na wengineo wote ambao ni wanakijiji tafadhalini naombeni sana mfikirie kwa kina na kuweka michango yenu ili tuwe na tija na ufanisi katika kuhakikisha kijiji chetu kinakuwa na manufaa kwetu na jamii nzima kwa ujumla.
Ni Changamoto tu, tupo kijijini kunufaishana na si kubezana na kurudishana nyuma!
Tags:
Shirikisha
-
▶ Jibu Hoja Hii