Nimekuwa nikiumizwa kichwa sana na tetesi kuwa kuna dawa/ sindano za kuongeza ukubwa wa baadhi ya viungo vya wasichana/ wanawake hasa hips na mawowowo. Nashindwa kujua kama ni kweli au c kweli, hebu nitoeni ushamba wa2 wangu nisije nikauvaa mkenge:
1) Niambie kama ni kweli hizo dawa/ sindano zipo.
2) Wapo wasichana wa kibongo wanatumia?
3) Je nitamjuaje msichana ambaye anatumia na asiyetumia? Watu tunataka vitu natural bwana, siyo artificial hahahaahaaaa.
4) Je kuna madhara yeyote kwa wanaotumia?
Ukiona hivyo Dis ujue madada wa fotobaraza si hao watumiaji wa vitu hivyo. Tuna maumbo ya natural sie! usipime mdogo wangu! ngoja nanihii wangu cherry aingie humo ndani halafu..., hahaha!
kwanza hongera mdogo wangu Dismas kwa kuanzisha mjadala wenye shule kibao! nakupa tano! :P
mdogo wangu dawa hizo zipo tu na kwa bahati mbaya kwetu Bongo zinauzwa kama pipi. Madhara yake si rahisi kuyajua sasa, lakini nyingi ya dawa hizo zimetengenezwa na mada zenye kusababisha magonjwa hasa ya Saratani. Na kwa kuwa inavyoonyesha makwetu bongo watu wanayatumia madawa hayo kwa wingi, basi katika miaka ijayo tukae tayari kusubiri mlipuko wa magonjwa ya ajabu ajabu hasa kwa wanawake.
Inasikitisha sana mtu kwa ajili ya kutafuta uzuri usio wa asili, ahatarishe afya yake kwa kiasi hicho. Inabidi uwe makini mdogo wangu. Wifi mwenye umbo la artificial simtaki mie!
Asante sana dada Waridi kww mchango wako bomba, Siyo cri mimi ningeweza kuuvaa mkenge. Lakini kwa sasa nimesha elimika vyakutosha, hakuna msichana wa kunidanganya kwa hilo. Sasa dada Waridi jiandae kupokea kifaa cha ukweli hahahaaaaa.