FotoBaraza.Net

Kuna habari imeripotiwa kuwa hadi sasa watu 12 ambao ni moja ya wapenzi wa mwanamuziki maarafu wa Pop duniani (Michael Jackson) aliyeaga dunia wiki iliyopita, nao wameamua kufupisha maisha yao kwa kujiua (commit suicide) sababu ya majonzi. Sizani Michael Jackson mwenyewe angependa kitu hiki kitokee kwa wapenzi wake.... Sijui wenzangu mnaonaje hoja hii...????

Kwa maelezo zaidi bofya hapa
http://news.sky.com/skynews/Home/UK-News/Michael-Jackson-Reports-Of...

Shirikisha Twitter

Jibu Hoja Hii

Michango ya Mjadala Huu

mama m nilitaka nikuulize kama ulikuwa bado hujakata tkt? kumbe nawewe unalo ok! ninini majaliwa ya hayo makaratasi mkononi ndio mtafanya kusamehe nakujumuisha kwenye rambirambi au nanyie mtadai kama desi na wanachama wao?

Jibu Hoja Hii

Araway..... Hilo karatasi nalitunza kama diamond wala sitaki refund. Tayari world leading collectors wameshaanza kuzitafuta hizo tickets kwenye internet, na wako tayari kuzinunua bei mara mbili tuliyolipia. Mwaka 2007 Kuna mtu London kauza ticket ya Elvis Presley kwa pound 7,000 (sawa na 14mil tsh) aliyonunua 1973.

Jibu Hoja Hii

Mwenzenu kamba ilikatika kabla ya kufikia lengo lenyewe!. maumivu niliyoyapata na kigugumizi cha kupumua kilichoniandama niliogopa kuchukua kamba ya pili na hivyo kusitisha zoezi zima la kumfuta the JACKO.

Jibu Hoja Hii

heheheheee!! pole weeee!! naona ulishabadilika rangi duh!

Jibu Hoja Hii

Pole sana Magere..... nafikiri roho mtakatifu alikushukia na kunena kwa lugha kabla ya kufikia lengo lenyewe ulilokusudia. Ila Cherry akija huko sijui kama kutakuwa na usalama. LOL............

Jibu Hoja Hii

Hahahahaha,Don umenivunja mbavu kweli kweli.Sasa unasemaje tukuletee ya plastic itakua soft kwenye ngozi na chance ya kukatika ni ndogo.

Jibu Hoja Hii

???????????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!????????????????????????????

CHA 29:7 na kuendelea

Jibu Hoja Hii

Mama M bongo pia wanajiua ila wenzetu wametuzidi wanaweza wakateketeza familia nzima kwa stress.Nakumbuka vizuri niko Forodhani secondary,msichana wa Foro primary alijiua sababu mvulana wa secondary kamuacha.Mama yangu mkubwa akaniuliza kwani wanaume wamekwisha? Kwahiyo watu wanaposhindwa kua na alternative ndio uchukua uamuzi huo.

Jibu Hoja Hii

Hawa wenzetu wanawake zao hawana mbungi kabisa wanapoachwa na wala hutosikia kajiua... sijui sababu wanawake ni mapepe sana????
Kujiua hapa na barani ulaya kote wanaume ndio wanaongoza, ukute hao wote waliojiua kwa ajili ya Michael Jackson 10 ni wanaume au ukute hakuna mwanamke kabisa. Sijui wana akili gani au ndio malezi tokea utoto wanashindwa kustahimili? Ujue hata sie bongo tuna stress kuzidi wao..... ukizingatia extended family zetu huko Africa basi wajikuta kila siku stress haziishi lakini tunastahimili. Wao wazungu wakuta ni mume, mke na mtoto (watoto), lakini shida ndogo tu ya kifedha (finacial melt down) mtu alishajipiga risasi. Lakini wewe unayezungukwa na extended family unajipa moyo, iko siku mambo yatajipa. Wala hufikirii kujiua.
Pia angalia watoto wa shule wanavyoua watoto wenzao kwa bunduki nchi zilizoendelea, watoto wa kibongo waliokulia shida hata siku moja sijasikia kaenda kuwatungua roho watoto wenzie darasani.

Jibu Hoja Hii

Kwa haraka haraka bongo wanawake ndio wanaoongoza kwa kujiua kuliko wanaume! kumbe ni kinyume na bara la Uropa

Jibu Hoja Hii

Hapa UK ni kila siku.... Soma habari hii baba kajiua kaacha mke na watoto wawili

http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/news/2514820/Dads-suicide-at-p...

Jibu Hoja Hii

nafikiri wana matatizo mengine katika maisha, wamekata tamaa sasa hicho kifo cha M.J ni kisingizio tu.

Jibu Hoja Hii

RSS

Besdei za Kuzaliwa

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter