FotoBaraza.Net

Kuna habari imeripotiwa kuwa hadi sasa watu 12 ambao ni moja ya wapenzi wa mwanamuziki maarafu wa Pop duniani (Michael Jackson) aliyeaga dunia wiki iliyopita, nao wameamua kufupisha maisha yao kwa kujiua (commit suicide) sababu ya majonzi. Sizani Michael Jackson mwenyewe angependa kitu hiki kitokee kwa wapenzi wake.... Sijui wenzangu mnaonaje hoja hii...????

Kwa maelezo zaidi bofya hapa
http://news.sky.com/skynews/Home/UK-News/Michael-Jackson-Reports-Of...

Shirikisha Twitter

Jibu Hoja Hii

Michango ya Mjadala Huu

Hatari hii!!! Niliwahi kusikia enzi za show zake watu walikuwa wakizimia kwa burudani! Yawezekana ni upenzi tu, kama wale wanaofia dini au siasa!

Jibu Hoja Hii

Nilihofu hili jambo lkn sikudhani litatokea,mmmhh!!! Mungu aniepushe na mapenzi hayo,nimekua mmoja walioingia huzuni sana kwa kifo chake ila sijafikiria kukatisha maisha yangu hawana uwezo wa ku deal na stress au grief ndio maana, na utakuta wangefiwa na ndugu zao wala wasingefanya hivyo.Pole kwa familia zao.

Jibu Hoja Hii

Cherry.... ujue hata waingereza ndio zao hizo. Wakuta kijana kajiua kisa kaachwa na girlfriend wake. Huwezi sikia kijana wa kibongo ajiua sababu ya girlfriend au mke wake.

Jibu Hoja Hii

Hao jamaa naona wanachukulia Maisha kirahisi sana.
Sijui ni Dini imekua pungufu?

Jibu Hoja Hii

Kaka yangu dini hawa walituletea lakini wao hawaifatilia kabisa. Hapa Uingereza makanisa mengi yameuzwa kuwa nyumba za kuishi watu, wakati huko bongo ndio kwanza waumini wa dini wanazidi kuongezeka na makanisa yanazidi kujengwa.

Jibu Hoja Hii

Hata bongo wapo wanaojiua sababu ya girl friend au boyfriend, ila huku ni mara chache na mara nyingi huwa tunawawahi kwa maziwa. Juzi juzi tu girl friend wa rafiki yangu alikula sumu baada ya kusikia boyfriend wake katoka zenj kaenda dar kwa mwanamke mwengine! Walimuwahi kumpeleka hospitali otherwise angejumuika na waliokufa na mikaeli jaksoni (RIP)

Jibu Hoja Hii

Ujue Pascal wengi wenye roho nyepesi za kujiua kwetu Africa ni wasichana na sio wanaume kama walivyo hawa wazungu. Hawa wanaume wenzenu kutoka machozi hadharani hata iwe ofisini (kazini) juu ya mwanamke ni jambo la kawaida.... Hukuti mwanaume wa bongo alilia mwanamke hadharani..

Jibu Hoja Hii

Pascal usemayo ni kweli lakini kunakuwa na ulakini ndani yake mtu anapofikia hatua hiyo..... wengine ukute wanakuwa hawana msimamo mzuri wa maisha ingawa sio wote

Jibu Hoja Hii

Hawana msimamo wa maisha, unamaanisha wameshakata tamaa, kwahiyo wanatafuta sababu tu ya kuondokea duniani au?

Jibu Hoja Hii

Ndio hivyo...

Jibu Hoja Hii

inahuzunisha sana kusikia habari hizo. mwenyewe nilikuwa nahali mbaya kusikia kifo cha mwana pop huyu lakini nashukuru kwa kupata capani la kutosha kunisahaulisha majonzi hayo la sivyo namimi ningekuwa kwenye hali mbaya! nilimpenda sana MJ.

Jibu Hoja Hii

Mie nilishtuka sana hadi leo siamini kwani nilikuwa najiandaa kwenda kumuona pale o2 Arena, ingawa baba M alikuwa ana mashaka sana na hiyo concert kutokana na afya ya Michael Jackson kwa ujumla tokea March.

Jibu Hoja Hii

RSS

Besdei za Kuzaliwa

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter