FotoBaraza.Net

CHA the Great

MWAKA 2009 UNAELEKEA KUISHA...NI KITU GANI KIMEKUFURAHISHA, KUKUHUZUNISHA, KUKUSHANGAZA AU KUKUKERA?

Amani iwe nanyi wote.

Ni mwezi wa 11 na zimebaki siku chache kuweza kukamilika kwa mwaka huu wa 2009. Kuna mengi yaliyotokea katika dunia hii, ya kusikitisha, kufurahisha na kukera au kushangaza. Wewe ni mambo gani yaliyokukera, kufurahisha au kukuhuzunisha?.
PamoJah

Shirikisha Twitter

Jibu Hoja Hii

Michango ya Mjadala Huu

Kwa upande wangu kwa mwaka huu, nilipatwa na simanzi pale nilipopata taarifa ya kifo cha rafiki yangu mpendwa (JOYCE MATIKU) rest in peace aliyefariki miezi michache iliyopita na aliacha mtoto wa mwaka mmoja. Pili ni pale nilipopata taarifa ya kupigwa makofi, ngumi na mateke ya rasharasha kwa Mzee wetu Alhaji Hassan Mwinyi na kijana mpuuzi. Vilevile habari za matukio ya kuuwawa kikatili kwa ndugu na jamaa zetu albinos. Kilichonifurahisha kwa mwaka huu ni pamoja na kukutana ana kwa ana na wanakijiji kama vile OSWALD aka HEAVY WEIGHT, dada MAJOY, mkuu YOUNG, PASCAL, MICHUZI JR.,DISMAS, ALFAN, ARAWAY, ANGEL NEHEMIA, NDEKIA, CHAOGA, MR. MAINGU, RT, DADA aka TYPIST, vilevile nilifurahi sana kupata simu toka abroad kwanza kabisa kutoka kwa LECTURE MAGERE, CHERRY, VADONDE na NYAU ,na wengine wengi ambao kwa kutaja majina yao hapa nitajaza kurasa. Lakini Namshukuru sana Mpenzi wangu kwa yote! Nampenda sana. Na support niliyopata toka kwa wadau wa FB na wale walio nje ya FB kwa kununua products zangu za PamoJah, kitu kilichonipa moyo wa kuendelea kuzalisha products hizi tena na tena. Thank you all, and GOD bless you all.
Hakuna kilichonishangaza kwa mwaka huu kwa sababau sikuzaliwa ili nishangae bali ku-reason, wewe kama unashangaa shauri yako, utashangaa hadi siku YESU KRISTU anarudi, na akikuuliza unashangaa nini wakati imeandikwa katika vitabu kuwa nitarudi sijui utamjibu nini!


PamoJah

Jibu Hoja Hii

Yani CHA hujafurahi kuonana na mimi?au tulionana mwaka jana?..SALAMA MOHAMED dadangu mpendwa sitakusahau aliponitoka mwaka huu burundi la kunifurahisha mpaka nishindwe kusahau mwaka huu ni pale nilipoambiwa nimeclear sup zangu...mengine ni kawaida kwa walalahoi kama mimi

Jibu Hoja Hii

Jamani Dear (Mtoto Mzuri) wewe si siku zote huwa tunaonana na kuongea on the phone. Mwa! Mwa!

Jibu Hoja Hii

Nimehuzunishwa na mwenendo wa siasa chafu za Tanzania, nimefurahi kuongeza/kukutana/kufahamiana na ndugu na jamaa katika kijiji cha FB. Nimekerwa na ubabaishaji unaoongezeka katika utendaji kwa kila sekta, kuanzia za serikali mpaka binafsi hata kwa mtu mmoja mmoja!

Jibu Hoja Hii

Ni kweli Mkuu Stiba. Mambo yanakwenda kama mchezo wa kuigiza katika nchi hii, yaani ni kama hakuna msimamizi mkuu.
PamoJah

Jibu Hoja Hii

Ufisadi ndio ulionikera kwa kiasi kikubwa.

Jibu Hoja Hii

Nitaongea kesho nikisharudi kutoka dar

Jibu Hoja Hii

Poa Mabagala!

Jibu Hoja Hii

2009 ni mwaka ambao umekuwa wa kufurahia maisha kwa upande wangu. Hasa kufurahia maisha na marafiki wapya kabisa. Cha kusikitisha ingawa si sana ni kupoteza simu nne sababu ya mambo yetu yale ya kwenye glasi. Pia ni kupata ajali ya gari kidogo nikitoka kwenye kinywaji mida ya usiku wa manane. Niligonga nguzo ya taa ya barabarani na kupata mikwaruzo kidogo sehemu za mkononi, ila sio mbaya. Kwa sasa ni hayo tu. kwa baadae nitarudi tena

Jibu Hoja Hii

Kila jambo linatokea kwa mapenzi ya mungu na kwa mwaka huu kama wengi mnavyojua nilipoetza mama na kwa kuwa mama ni mmoja tu duniani pengo lake ni gumu sana kuzibika na nitaendelea daima kukumbuka mwaka huu kwa miaka yote niliyobakiza,na pia kufika kwangu nyumbani nimeonana na wadau wengi na kwa wale mliofika nyumbani sina cha kuwalipa wakati ule na nimeamini rafiki wa kweli utamuona kwenye shida,na wale wote walioacha ujumbe wa matumaini na salamu,sina cha kuwalipa ninawaombea muweze kuendelea na upendo huo huo.
Kwa kuwa mwezi november ni wa kukumbuka marehemu wote basi naomba tuwakumbuke marehemu wote kwa sala hii:
Eternal rest give to them,O Lord and let perpetual light shine upon them.
May they rest in peace.May the soul of the faithful departed through the mercy of God rest in peace.
Amen.

Jibu Hoja Hii

Amen Mkuu Young!

Jibu Hoja Hii

Amen Young

Jibu Hoja Hii

RSS

Besdei za Kuzaliwa

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter