Ni mwezi wa 11 na zimebaki siku chache kuweza kukamilika kwa mwaka huu wa 2009. Kuna mengi yaliyotokea katika dunia hii, ya kusikitisha, kufurahisha na kukera au kushangaza. Wewe ni mambo gani yaliyokukera, kufurahisha au kukuhuzunisha?.
PamoJah
Kwa upande wangu kwa mwaka huu, nilipatwa na simanzi pale nilipopata taarifa ya kifo cha rafiki yangu mpendwa (JOYCE MATIKU) rest in peace aliyefariki miezi michache iliyopita na aliacha mtoto wa mwaka mmoja. Pili ni pale nilipopata taarifa ya kupigwa makofi, ngumi na mateke ya rasharasha kwa Mzee wetu Alhaji Hassan Mwinyi na kijana mpuuzi. Vilevile habari za matukio ya kuuwawa kikatili kwa ndugu na jamaa zetu albinos. Kilichonifurahisha kwa mwaka huu ni pamoja na kukutana ana kwa ana na wanakijiji kama vile OSWALD aka HEAVY WEIGHT, dada MAJOY, mkuu YOUNG, PASCAL,MICHUZI JR.,DISMAS, ALFAN, ARAWAY, ANGEL NEHEMIA, NDEKIA, CHAOGA, MR. MAINGU, RT, DADA aka TYPIST, vilevile nilifurahi sana kupata simu toka abroad kwanza kabisa kutoka kwa LECTURE MAGERE, CHERRY, VADONDE na NYAU ,na wengine wengi ambao kwa kutaja majina yao hapa nitajaza kurasa. Lakini Namshukuru sana Mpenzi wangu kwa yote! Nampenda sana. Na support niliyopata toka kwa wadau wa FB na wale walio nje ya FB kwa kununua products zangu za PamoJah, kitu kilichonipa moyo wa kuendelea kuzalisha products hizi tena na tena. Thank you all, and GOD bless you all.
Hakuna kilichonishangaza kwa mwaka huu kwa sababau sikuzaliwa ili nishangae bali ku-reason, wewe kama unashangaa shauri yako, utashangaa hadi siku YESU KRISTU anarudi, na akikuuliza unashangaa nini wakati imeandikwa katika vitabu kuwa nitarudi sijui utamjibu nini!
Yani CHA hujafurahi kuonana na mimi?au tulionana mwaka jana?..SALAMA MOHAMED dadangu mpendwa sitakusahau aliponitoka mwaka huu burundi la kunifurahisha mpaka nishindwe kusahau mwaka huu ni pale nilipoambiwa nimeclear sup zangu...mengine ni kawaida kwa walalahoi kama mimi
Nimehuzunishwa na mwenendo wa siasa chafu za Tanzania, nimefurahi kuongeza/kukutana/kufahamiana na ndugu na jamaa katika kijiji cha FB. Nimekerwa na ubabaishaji unaoongezeka katika utendaji kwa kila sekta, kuanzia za serikali mpaka binafsi hata kwa mtu mmoja mmoja!
Kila jambo linatokea kwa mapenzi ya mungu na kwa mwaka huu kama wengi mnavyojua nilipoetza mama na kwa kuwa mama ni mmoja tu duniani pengo lake ni gumu sana kuzibika na nitaendelea daima kukumbuka mwaka huu kwa miaka yote niliyobakiza,na pia kufika kwangu nyumbani nimeonana na wadau wengi na kwa wale mliofika nyumbani sina cha kuwalipa wakati ule na nimeamini rafiki wa kweli utamuona kwenye shida,na wale wote walioacha ujumbe wa matumaini na salamu,sina cha kuwalipa ninawaombea muweze kuendelea na upendo huo huo.
Kwa kuwa mwezi november ni wa kukumbuka marehemu wote basi naomba tuwakumbuke marehemu wote kwa sala hii: Eternal rest give to them,O Lord and let perpetual light shine upon them.
May they rest in peace.May the soul of the faithful departed through the mercy of God rest in peace.
Amen.
Permalink Reply by Dada on Novemba 14, 2009 at 8:55am
Jamani kwanza kilichonifurahisha mwaka huu ni kukutana na wanakijiji kadhaa katika party ya kuzaliwa kwa FB tarehe 7 February, 2009 pale Mgahawa wa Soma nikianza na Araway, Babukadja, Bibi (Mke wa Babukadja), Ndekia, Michuzi Jr, Alma and her husbamd, Mtoto Mzuri, Bbland, Ma Joy, Dr. Stiba, Chaoga, RT, MC wetu wa siku ile Maingu, jamani walikuwa wengi sana siku ile mniwie radhi kwa wale ambao sikuwataja. Nawashukuru sana kwa kila jambo tulilo share!!! Pia niliweza kukutana na huyumuanzisha mjadala huu CHA aka MPIGA JEKI. Nilifurahi sana kwa kuongeza Idadi ya NDUGU JAMAA na MARAFIKI kutoka FB.
Jambo lingine lililonifurahisha mwaka huu jamani kwa kufaulu vyema mitihani yangu ya Degree ya Pili ya Mawasiliano ya Umma na Mungu akinipa uhai Novemba 28, 2009. I THANK GOD for that.
Jambo lililonisikitisha na kunihuzunisha, kunishangaza na kunikera kwa mwaka huu ni siku nilipofika chumba cha mtihani wangu wa mwisho wa kumaliza masomo na kukuta hakuna mtihani eti kwa sababu Lecturer wa somo hilo hayupo nchini kwa hiyo tutafanya atakarudi.
Pia nawaombea wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki pumziko la Amani milele Amina, akiwemo YOUNG na MTOTO MZURI kwa kupoteza mmoja wa wazazi wao. AMINA.