FotoBaraza.Net

Don Magere

Miaka 40 ya internet!!je nilini ulipata e-mail adress yako?

E-mail adress yangu ina miaka 11 hadi sasa.Nakumbuka jinsi nilivyokuwa na furaha mara baada ya kufungua adress yangu ambayo mpaka leo sijawahi kuibadilisha.Kuwa na e-mail adress kumejenga daraja kubwa na refu katika maisha yangu na marafiki zangu.
Je wewe mwanakijiji E-mail adress yako ina umri gani? na ulijisikiaje mara baada kuweza kuwasiliana kwa njia ya internet?

Shirikisha Twitter

Jibu Hoja Hii

Michango ya Mjadala Huu

nami pia ina miaka 11, ingawa bahati mbaya ina 2000 pale kwa kuwa nilikuwa napenda sana mwaka 2000 ufike
nilijiona kama supa staa, nakumbuka niliifungua huku natetemeka nilikuwa najua siri zangu za maisha zitajulikana na wazungu, nikawa nikitumiwa email yeye picha ya kikubwa nafuta haraka nisionekane mhuni kwa wazungu.

Jibu Hoja Hii

ha ha ha MUJYDEBUBYZ umenichekesha sana mkuu wangu!

Jibu Hoja Hii

ha ha ha ah ah h Don ilikuwa balaa, nilikuwa najua wazungu wanachunguza mambo yangu kwa email

Jibu Hoja Hii

mambo mengi sana

Jibu Hoja Hii

DUH BROTHER DON,SWALI LAKO HILI LINANIFANYA NIDONDOSHE HAPA CHINI YAFUATAYO:
ZAMANI NILIKUWA NIKITAMANI SANAKUWASILIANA KWA KUTUMIA NJIA YA EMAIL,NILIPOKUWA KUWA NIKIONA MTU ANAKWENDA I..CAFE AKISEMA KWAMBA ANAKWENDA KUMTUMIA UJUMBE RAFIKI YAKE,NILIKUWA NAJISIKIA MACHUNGU KAKA,NIKAWA NIKIIULIZA NAFSI YANGU NILINI NA MIMI NITAMILIKI EMAIL ADRESS?NAFSI YANGU ILIKUWA IKINIPATIA JIBU KWAMBA USIWE NA TABU,UTAFANIKIWA TU SIKU MOJA!LAKINI KIPINDI HICHO ILIKUWA NI VIGUMU SANA KUWEZA KUKAMILISHA NDOTO YANGU HIYO YA MUDA MREFU.NA HII NI KWA SABABU KIPINDI HICHO NILIKUWA NAKAA KIJIJI,KAMA UNAVYOJUA HUKO INTERNET NI TABU KWELI,LAKINI BAADA YA KUMALIZA DARASA LA SABA MWAKA ELFU 2000,NIKAHAMIA JIJI DAR ES SALAAM,HUKO NILIKUTA KILA KITU CHEPESI ,INTERNET KIBAO KILA KONA,BASI SIKU MOJA NIKAINGIA NA UNCLE YANGU KATIKA INTERENET MOJA INAYOPATIKANA PALE MAENEO YA AKIBA KWENYE MJENGO MKUBWA AMBAO JUU YAKE KUNA PARKING YA MAGARI,NIKAWEZA KUFUNGUA EMAIL YANGU TUKUFU,EMAIL YA KWENZA KUFUNGU ILIKUWA NI YAHOO,NA HII NI KWA SABABU EMAIL ILIYOKUWA FAMOUS KATIKA UBONGO WANGU ILIKUWA NI YAHOO MAIL.NILIANZIA HAPO KUTUMIA EMAIL YA HOO KWA KUWASILIANA NA JAMAA NA MARAFIKI.LAKINI BAADA IKAWEPO HALI YA MAENDELEO KIDOGO,KWANI NILIWEZA KUGUNDUA KUWA NI AINA KADHA ZA EMAIL ADRESS,KAMA VILE GMAIL,HOTMAIL,ULIPOFIKA MWAKA 2004,NIKAAMUA KUFUNGUA EMAIL MPYA YA (GMAIL) MAANA ILE YA YAHOO KUNA WAKATI ILIKUWA IKINICHANGANYA ,NIKIDOWNLOARD BAADHI YA VITU INAKUWA NGANGALI KINOMA MPAKA NIKAWA NIKIWAGOMBEZA WAMILIKI WA INTERNET CAFE NIKIDHANI WANANIIBIA MUDA WANGU HASA PALE WANAPONIHESABIA WAKATI NA KUNIAMBIA NILIPE KIWANGO CHA JUU,KUMBE HIYO ILIKITOKANA NA KUZOROTA KWA YAHOO KAMA VILE WAKATI WA KUSEND AU KUOPEN,HUWA HAICHANGAMKI.NDIPO MWAKA HUO WA 2004 NILIPOAMUA KUWA NA EMAIL YA PILI NAYO NI {GMAIL.COM} HIVYO NIKAUMBA EMAIL YANGU INAYOKWENDA NAMNA HII:

(taqee07@gmail.com),na ile ya mwanzo,ilikuwa hii:(tzchalii@yahoo.com).mpka sasa natumia zote mbili lakini ambayo naitumia sana ni ile ya gmail kwa sababu inajua maisha hasa unapokuwa katika internet isiyokuwa ya kwako kwani iko faster kudownloard ,kusend,na kuopend pamoja na kusearch.

hivyo yahoo yangu inaumri wa miaka (9) na gmail yangu ina umri wa miaka (5),lakini nashukuru sana mwenyeezi mungu aliyenipa fikra ya kufungua adress hizi mbili maana mpaka zimeniletee mafanikio makubwa sana kama vile kunikutanisha na marafiki mbalimbali kila pembe ya dunia na ndani ya taifa langu,leo hii nikishuka bongo nakuta kuna marafiki zangu kibao,tunakutana kufurahi na kuenjoy utadhani mtu na kaka yake au mtu na dada yake,hii yote ni kwa sababu ya faida ya mawasiliano kw anjia ya email kupitia FOTO BARAZA!!

PONGEZI KWENU WANA FOTO BARAZA MLIOZITUMIA EMAIL ZENU KUJIUNGA NA KIJIJI HIKI CHENYE LENGO LA KUWAKUTANISHA WATANZANIA POPOTE PALE WALIPO ULIMWENGUNI NJE YA NCHI NA NDANI YA NCHI KUWAFANYA KUWA PAMOJA KAMA WANANDUGU AU WATU WA JAMII MOJA.


MBARIKIWE:

Jibu Hoja Hii

Mkuu umenikumbusha mbali kwa kweli email yangu ina miaka12 sasa,kwanza naithamini sana maana kila ninayempa anakubali mi wa kitambo don town,pili umenikumbusha excite.com,usa.net dah kitambo kweli ila tumepata marafiki wengi kupitia emai tunamshukuru Mungu!

Jibu Hoja Hii

RSS

Besdei za Kuzaliwa

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter