E-mail adress yangu ina miaka 11 hadi sasa.Nakumbuka jinsi nilivyokuwa na furaha mara baada ya kufungua adress yangu ambayo mpaka leo sijawahi kuibadilisha.Kuwa na e-mail adress kumejenga daraja kubwa na refu katika maisha yangu na marafiki zangu.
Je wewe mwanakijiji E-mail adress yako ina umri gani? na ulijisikiaje mara baada kuweza kuwasiliana kwa njia ya internet?
mimi email adress yangu ina miaka saba,
nilifurahi kuipata na niliahangaika wiki nzima kuitengeneza.ila baada ya miaka minne nikaacha kuitumia nikatengeneza ya mtandao mwingine.ila baadae nikagundua hii ya kwanza ndo ilikua mzuka zaidi.basi nikairudia tena,hadi leo nnaifurahia ilinihuzunisha mara chache tu lakini kwa kiasi kikubwa inanifanya nifurahi.imenifahamisha na mengi na wengi na vingi.
Email address yangu yangu ya kwanza ina miaka 10, ni kweli imenikutanisha na watu wengi sana mkiwemo nyie wanafotobaraza, pamoja na wadau wengi tu duniani. Baada ya kuanza kujua uzuri wa email, mpaka leo sijaandika barua tena,. Nilikuwa napenda sana kutuma post cards na greetings cards, lakni baada ya kufungua email address yangu mpaka leo sijafanya tena hayo mambo. Na baada ya kujua utamu wa email nakumbuka nilikuwa sikosekani pale Shangani Internet Cafe ( Zanzibar). Kila nikitoka shule ilikuwa lazima nipite pale. Imenikutanisha na watu wengi wakiwemo nyinyi. Wengine nimeonana nao na wengine nawasiliana nao tu sijaonana nao. Nina hakika bila haka ka email ka yahoo na hotmail, na sasa gmail, basi wengi wenu nisingewajua. Kumbe internet ina miaka 40 sasa? sikuelewa hiki kitu!
Mimi yangu ina miaka 5 tu, Niliifungua nikiwa mitaa ya kati baada ya kuua 4m4, nilijisikia mtu wa maana sana hasa ukizingatia nilikuwa napenda kuchart na rafiki zangu kwa barua hii ikaniweka juu. Imenifanyia mambo mengi hadi sasa haswa haswa imenikutanisha na marafiki mbali mbali kama hapa fotobaraza, ispokuwa kuna mtu alijaribu kuifungua na kutumia as me...sasa sijui aliifungua kivp alinifanya nipate wasi wasi na kufungua nyingine. Baadae nikaona nisiache mbachao kwa msala upitao nikarudi kuiset upya na kila kitu kikawa shwari
Dah .naishukuru saaaaaana mana imenikutanisha na wengi wengine ndugu zangu, classmate na wengine wengi ambao nilikuwa nimewapoteza , siongei mengi naomba niishie hapa mana nitalia......
Thanx
Du!! Umekumbusha mbali..... email address yangu (hotmail) nilifungua 1997 nikiwa chuoni na ndio naitumia hadi leo. Inanifanya niwasiliane na ndugu, jamaa, marafiki & old classmates pembe zote za dunia kwa miaka 12 na uchafu. Pia nina Yahoo ambao nimeifungua last year.
Nakumbuka mara ya kwanza nilipojua kutumia internet kama njia ya mawasiliano ilikuwa darasani... kama ujuavyo mambo ya wanafunzi tulikuwa tunatumiana vi-pop up msges (intranet) kwenye screen kama njia ya mawasiliano mkitaka kwenda lunch, coffee break au kusikia una boreka na kipindi, basi lecturer/Professor akiwa karibu yako wafuta private msges zote na kujifanya uko busy kweli kweli kwenye screen yako kumbe uwozo mtupu. LOL.....
Ebwana mimi na miaka 8 natumia email yangu
na nilishawahi kufungua email kwenye
mitandao mi lakini mpaka sasa natumia email
yangu ya mwazo izo zingine nisha zisaahu
MMMH MIE MIE MIE MEIE email yangu ya kwanza ya hotmail mpaka sasa imetimiza miaka 9, ingawa ninayo tumia sana kwa sasa ni ya gmail, lakini kwakweli hotmail naipenda sana kwa sababu haina kikorombwezo chochote mbele ni jina langu kamili chaoga@hotmail.com, bwana magere asikwambie mtu kipindi kile net ilikuwa nusu saa 500 lisaa limoja 700 halafu iko slooow