Wadau wapendwa,
kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kukutana kwa baadhi ya wadau katika kikao kilichofanyika tarehe 17/10/2009 pale Best Bite,Namanga.Japo tulikuwa wachache sana lakini tuliweza kuzungumza na kufikia muafaka wa jinsi itakavyokuwa siku hiyo ya Tarehe 07/11/2009
katika kikao kilichofanyika tarehe 17/10/2009 kilipendekeza kwamba itakuwa ni vizuri zaidi kwa siku hiyo ya tarehe 07/11/2009 kuwa ni siku ya kukutana kwa kufahamina na kubadilisha na mawazo pia kujadili mambo mbalimbali ya kijiji,jambo ambalo liliafikiwa na wadau wote waliohudhulia katika kikao hicho.ambapo Msasani Beach Club ndiyo sehemu iliyopendekezwa kwa kufanyia shughuli hiyo.
hivyo basi tulikubaliana kuwa hakutakuwa na michago ya aina yeyote ila badala yake kila Mdau ataruhusiwa kujihudumia mwenyewe kutokana na mfuko wake ulivyo. kwa hiyo tunatakiwa kufika bila kukosa siku hiyo ya tarehe 07/11/2009 pale Msasani Beach Club kuanzia saa nane unusu (14:30) mchana.
Kila la kheri kwenye hiyo sherehe au mkusanyiko mtakao kuwa nao,tunawatakia shughuli njema na yenye baraka na mafanikio tele,hatutakuwa pamojah lakini, tutakuwa pamojah kwenye lolote mtakalo kuwa mmepanga,wale wa uk mama Malaika alishauri tukutane wapi tumefikia wadau?Pamojah tunaweza.