CHA kipindi cha nyuma ulikuwa makini katika kukosoa wale wote wenye matumizi mabovu ya kiswahili lakini kwa sasa umeacha kazi hiyo. Kiswahili kibovu kimeibuka kwa kasi ya ajabu kama wamachinga walivyorudi katika mitaa ya Kariakoo na kule kati posta.
CHA chukua RUNGU lako ulilokabidhiwa na kijiji ili uwashikishe adabu hawa wachafuzi wa Lugha.(hapa simaanishi kiswahili cha kihuni)
Ni kiswahili hiki cha kawaida ambacho kwa mfano badala ya mtu kuandika
ADHA anaandika HADHA
HIZI anaandika IZI
AIBU anaandika HAIBU
DHARAU anaandika ZARAHU
Kuna mengi zadi ila nimetaja machache tu
Inakera sana na inakatisha tamaa kusoma maoni ya mtu kama makosa ya namna hiyo yanajirudiarudia.
Chonde chonde CHA take action please!
Makosa ni kawaida hata mimi kuna mambo nayokosea, lakini wengine ni wabishi yaani wao hawataki kusahihishwa si katika Kiswahili au Kiingereza (English). We nambie hivi kuna mwalimu ambaye anafundisha mtu kusema "KWA NIABA YANGU" au "CHUKI BINAFSI" hii ni lahaja ya wapi?.
Ni kweli promota usemayo lkn nahisi iwe jukumu la wote kurekebisha makosa hayo.Kuna siku nilikua naangalia picha ya mdau mmoja hapa ilikua niache maoni kua picha yake nimeipenda maana alitoka bomba lkn mdau mwengine alikua kashaacha maoni akiieleza picha hio maneno yalikua hivi "dada huna sura nzuri" akimaanisha dada una sura nzuri.Ilinivunja nguvu nikatoka bila kuacha maoni.Na kipindi hiki kumezidi makosa hayo sasa sijui kama ni kutokurudia kusoma ulicho kiandika au watu tu hawajui tofauti ya baadhi ya maneno?????