CHA kipindi cha nyuma ulikuwa makini katika kukosoa wale wote wenye matumizi mabovu ya kiswahili lakini kwa sasa umeacha kazi hiyo. Kiswahili kibovu kimeibuka kwa kasi ya ajabu kama wamachinga walivyorudi katika mitaa ya Kariakoo na kule kati posta.
CHA chukua RUNGU lako ulilokabidhiwa na kijiji ili uwashikishe adabu hawa wachafuzi wa Lugha.(hapa simaanishi kiswahili cha kihuni)
Ni kiswahili hiki cha kawaida ambacho kwa mfano badala ya mtu kuandika
ADHA anaandika HADHA
HIZI anaandika IZI
AIBU anaandika HAIBU
DHARAU anaandika ZARAHU
Kuna mengi zadi ila nimetaja machache tu
Inakera sana na inakatisha tamaa kusoma maoni ya mtu kama makosa ya namna hiyo yanajirudiarudia.
Chonde chonde CHA take action please!
Lugha/maandishi matamu humvutia msomaji, haswaa sisi tuliosoma muandiko na sarufi! Kiukweli wengi wetu hudharau sana kile tuandikacho, na hiyo inaonesha kuwa huwa tunaandika bila kurejea maandishi yetu kabla ya kuyaweka kwa ajili ya kusomwa na wadau wengine. Tujitahidi kuandika vizuri ili kutupa ladha ya kile kiandikwacho!
Umesema kweli Mkuu Stiba. Unajua kuna mambo mengi tu huwa nawasikia hata wale waitwao waheshimiwa pale bungeni. Kwa mfano utamsikia mbunge akisema "kwa niaba yangu" na "kwa niaba ya fulani", kweli hivi hiki ndicho Kiswahili tulichofundiswa darasani na walimu wetu kweli? Au haya ni matokeo ya kufundishwa na walimu ambao walifeli?
Tatizo letu watanzania huwa tunajifanya tunaongea "slang" ya kiswahili, wakati hata kiswahili chenyewe fasaha hatukijui! Kwa mfano ukitaka kusikiliza kiswahili fasaha uwe mtazamaji wa kipindi cha lugha yetu cha TBC1 uwasikilize kina Mochiwa na wenzie wanavyoongea kiswahili mpaka utasikia raha!
Tatizo bado tunataka kuongea Kiswahili kwa kufananisha na lugha ya Kiingereza (English). Wewe wasikilize watangazaji mbalimbali hasa wa hizi radio binafsi wanavyoharibu Kiswahili, na hawa ni chanzo cha kupotosha kiswahili, wengine ni wabunge yaani mimi huwa nacheka sana mkuu Stiba, hata humu ndani wamo wengi sana, sasa kwa mfano maneno kama hayo yaliyoorodheshwa na Lecturer Magere kweli yanatia hasira sana, eti mtu na kwa nguvu zote na kwa kujiamini anasema HAIBU badala ya AIBU, ZARAU badala ya DHARAU na mengine mengi tu.
Dawa yao ni kumpa Lecture Magere kazi ya "Kifimbo cheza", kila atakaeharibu lugha ama kwa kuandika au kwa kuongea atachezea bakora mpaka anyooshe! Au unaniambiaje mkuu CHA?1
Ni kweli Dr Stiba mwandiko wako ni mzuri, maana ni kama vile unapigisha chapa. Nakumbuka notice zako zilivyokuwa zikisambaa, kila mtu akipenda kusoma maandishi yako na ya God Sula.