FotoBaraza.Net

Jamaa ambaye ni mkurugenzi wa kampuni moja kubwa ya mawasiliano alikaribishwa kutoa speech katika tamasha moja la vijana lililokuwa limeandaliwa kuhusu kujiepusha na vitendo vyenye kuweza kusababisha maradhi ya kisasa.Speech ya mkurugenzi huyu ilinukuliwa kama ifuatavyo:
Hali ngumu sana vijana kwasababu kila mmoja anataka kuonja uzuri wa maisha ya kisasa.Mtandao wa ugonjwa huu ni mkubwa,mimi nashauri muwe makini.Jitahidini sana kukaa bila kupiga......Ni muhimu simu zenu mzitunze sana na wala si kupiga piga kwani hii ni hatari na gharama yake ni kubwa.Kama shida ya kupiga itakuwa ni kubwa basi hakikisha simu yako iko kwenye kipochi.na hivi vipochi vinapatikana kwa wingi na gharama yake si kubwa.Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata maradhi yanayoweza kusababishwa na mionzi iliyoko katika simu hizi za kisasa.Ni mwiko kabisa kupiga Vodacom kwa Vodacom kwani hii ni hatari kubwa mno.
Watu wengi simu zenu zina fanya kazi vizuri tu na mna hamu angalau ya kubipu,lakini hii nayo ni hatari,kwani mwenzako akionyesha utashi wa kupokea ni rahisi sana kwako kuamua kupiga kabisa.Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu,eti simu zenu zitamaliza chaji, hii si kweli.hakikisha tu kwamba simcard iko katika hali nzuri, hi ndio ina kumbukumbu zote na ndio inayoongoza mawasiliano yote.
Simu ni simu tu, na madhumuni yake yanafanana.Usidanganyike na simu eti ina camera au double screen hizo ni mbwembwe tu.Kuna simu nyingi sana na feki siku hizi zinauzwa zimevishwa cover mpya,USIDANGANYIKE. Ukiona maisha bila kupiga hayawezekani basi tafuta sehemu inayoaminika na uwe unapiga hapo tu, hi itasaidia sana kwani simu ukitumia peke yako inadumu zaidi kuliko ile yenye subscribers wengi.
Alihitimisha kwa kuwasisitiza kuwa vijana wabadili tabia kwa kuacha kupigapiga ovyo simu.....
Mh sijui mnasemaje kuhusiana na speech hii..........................................

Shirikisha Twitter

Jibu Hoja Hii

Michango ya Mjadala Huu

Mh!

Jibu Hoja Hii

hahahahahhaaa! Alikuwa anamaanisha kupiga simu kweli au kuna kingine anachoogopa kutaja?????

Jibu Hoja Hii

RSS

Besdei za Kuzaliwa

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter