FotoBaraza.Net

CHA the Great

ALFANI APATA ZAWADI YAKE KATIKA SHINDANO LA *SHINDA MUDA WA MAONGEZI WA 50000/- (ELFU HAMSINI) AU LUNCH HOTEL YA KILIMANJARO 'MARUDIO' ZAWADI IMEONGEZWA*.

Kwanza kabisa naomba radhi kwa usumbufu uliotokea kwa Bw. Dismas na wanakijiji kwa ujumla kutokana na hitilafu ya lugha. Kutokana na malalamiko ya wadau tumekubaliana kuwa shindano hilo lirudiwe. Na mdhamini wa shindano hili ameahidi kuongeza zawadi ya muda wa maongezi kutoka 30000/- hadi 50000/- za Kitanzania. Katika shindano hili majina yafuatayo hayatoruhusiwa kushiriki katika shindano hili kwa kujibu maswali. Majina hayo ni Michuzi Jr. ambaye ni Balozi, Oswald Akyoo ambaye ni Mdhamini, Dismas, Cha, ambaye ni muanzilishi wa PamoJah na Mkuu au Mwenyekiti wa kijiji hiki Babukadja.

Maelezo mafupi juu ya maswali. Andika herufi unayoona ni sahihi katika kila swali au andika SI KWELI kwa swali unarofikiri halina usahihi na KWELI katika swali unalofikiri ni sahihi na kujaza sehemu iliyowazi au kutaja kinachotakiwa kutajwa.

1.Mwanachama yupi alitoa wazo la kuchapishwa t-shirts za PamoJah? A. Babukadja B. Dismas C. Michuzi Jr.
2. Taja majina mawili ya wana PamoJah waliopewa onyo kutokana na utovu wa nidhamu hapa kijijini.
3. Taja majina 15 ya wanachama wa PamoJah waliojiunga Baada ya Tarehe 23-Dec-2009.
4. A. Magere B. Mujydbubz C. Lucie wa Mama, D. Vadonde, E. George Rutenge mmoja wao ni wa kwanza kuvaa t-shirt ya PamoJah.
5. Chaoga, Mtoto Mzuri, Pascal, Ndekia, Michuzi Jr. Dismas ni wanachama wa PamoJah kwa sasa.
6. Taja jina la Muanzilishi wa FOTOBARAZA FONDATION.
7. Taja jina halisi la Mkuu wa Malavidavi ( Love Affairs)
8. Young alitembelewa na wana PamoJah 5 waliokwenda kumpa pole kutokana na msiba wa mama yake (YOUNG), taja majina yao.
9. Taja jina la msanii wa kiume aliyewahi kuonekana katika mchezo wa kuigiza akiwa amevaa T-shirt ya PamoJah katika kituo cha ITV.
10. Taja jina la msanii wa kike aliyewahi kuonekana amevaa t-shirt ya PamoJah katika mchezo wa kuigiza katika kituo cha ITV.

SHINDANO HILI LITAISHA SIKU YA ALHAMISI TAREHE 17-9-2009, SAA SITA MCHANA
KUJIBU MASWALI NI MARA MOJA TU, MSHIRIKI ATAKAYESHIRIKI ZAIDI YA MARA MOJA ATAKUWA AMEJITOA KATIKA SHINDANO HILI. ZAWADI KUTOLEWA NA MDHAMINI WA SHINDANO HILI, BWANA OSWALD JOHN AKYOO.
ZAWADI HAITABADIRISHWA KWA FEDHA.

PamoJah
na senksi so mach indidi!!!

Shirikisha Twitter

Jibu Hoja Hii

Michango ya Mjadala Huu

Asanteni wote kwa kushiriki kwa mara nyingine katika shindano hili. Kwa wale wanaofikiri kuwa kuna dosari ya maswali naomba wasome maelezo hayo hapo chini katika rangi ya blue ambayo ni maelezo yaliyopo katika maelekezo ya kujibu maswali.
Maelezo mafupi juu ya maswali. Andika herufi unayoona ni sahihi katika kila swali au andika SI KWELI kwa swali unarofikiri halina usahihi na KWELI katika swali unalofikiri ni sahihi na kujaza sehemu iliyowazi au kutaja kinachotakiwa kutajwa.

Na ninapenda kuchukua nafasi hii kusema ya kuwa tusitumie mahala hapa kama sehemu ya kupakana matope. Nimesoma comments zote na nimezielewa vizuri sana, hayo yamekwisha, ila vilevile nasikitika sana kwa uamuzi wa mtu nisiyemfahamu kunitukana kwa kupitia SMS. Haya ni mambo madogo sana, sasa inapofikia hatua ya watu kuanza kutukanana inakuwa haipendezi.

Na kutokana na majibu yenu washiriki mliojibu maswali haya, ni Alfan pekee ndiye aliyejibu maswali yote.
Nachukua nafasi hii kumtangaza Alfan kuwa ndiye mshindi wa shindano hili, na utaratibu unafanyika ili uweze kupata zawadi yako.
Asanteni sana..........

Jibu Hoja Hii

Narudi kusema tena maswali yote yaliandaliwa na sijakurupuka.

PamJah

Jibu Hoja Hii

sawa lkn roho inauma mtu hukutaka kunielewesha japo kidogo!

Jibu Hoja Hii

asante sana kaka CHA.
mimi pepsi zangu mbili kwa mshindi bado zipo palepale.
kidumu chama cha fotobaraza,idumu PAMOJA.

Jibu Hoja Hii

Asante RT.
Tupo PamoJah

Jibu Hoja Hii

hivi sasas ni saa sita na dakika 47 nilikuwa najiandaa kujibu maswali kabla ya muda kikomo kuisha lakini naona mshindi keshatangazwa. sijui nikate rufaa??

bwana magere naomba uwe wakili wangu nikatapo rufaa!!

Jibu Hoja Hii

Ha ha ha! Araway siwezi kujua saa yako na ya mwandaa shindano kama zinatunza muda sawa!
Hivyo nakushauri usikate rufaa maana chance ya kushinda ni minus100%

Jibu Hoja Hii

Kwanza Hongera Alfan kwa kuibuka kidedea katika shindano hili!

Pili nampongeza mwandaaji wa shindano hili kwa busara zake maana ametulia hata pale kulipotokea mikikimikii ya Lugha na matumizi yake aliweza kusimaa kidete nahatimae shindano limemalizika salama.
Kwa waliotumia lugha mbaya dhidi ya mwandaaji jamani huo sio ungwana na hata wale waliodriki kumtukana kupitia sms pia huo sio uungwana.
Tukumbuke huyu CHA anatumia muda wake na utashi wake kukiweka kijiji hiki live hivyo hakuna chochote anachofaidika nacho zaidi ya kutuchangamsha na kutuburudisha.
CHA usikate tamaa na hii uichukue kama changamoto tu kwako! kumbuka penye wengi kuna mengi pia.Tunatarajia tutaendelea kuburudika na mashindano yako hata siku zijazo.
Pamojah

Jibu Hoja Hii

Asante Lecturer kwa kutambua mchango wangu.

PamoJah

Jibu Hoja Hii

Hongera sana ALFAN kwa ushindi. Nadhani hakuta kuwa na mgogoro wowote juu ya ushindi wako.

Jibu Hoja Hii

mmmh wengine ndio hatujashirikishwa kabisaaaaaaaaaa yawezekana mi sio mwana kijiji teh teh, Hongera Alfan

Jibu Hoja Hii

Ha ha ha Dada Candy tatizo unaingia kijijini kwa ku-beep, ndo mana mengi yanakupita. But usikate tamaa, mambo mengi na makubwa yanakuja.

PamoJah

Jibu Hoja Hii

RSS

Besdei za Kuzaliwa

© 2010   Created by Babukadja on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Report an Issue  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!
Free Web Counter
Hit Counter