Kwanza kabisa naomba radhi kwa usumbufu uliotokea kwa Bw. Dismas na wanakijiji kwa ujumla kutokana na hitilafu ya lugha. Kutokana na malalamiko ya wadau tumekubaliana kuwa shindano hilo lirudiwe. Na mdhamini wa shindano hili ameahidi kuongeza zawadi ya muda wa maongezi kutoka 30000/- hadi 50000/- za Kitanzania. Katika shindano hili majina yafuatayo hayatoruhusiwa kushiriki katika shindano hili kwa kujibu maswali. Majina hayo ni Michuzi Jr. ambaye ni Balozi, Oswald Akyoo ambaye ni Mdhamini, Dismas, Cha, ambaye ni muanzilishi wa PamoJah na Mkuu au Mwenyekiti wa kijiji hiki Babukadja.
Maelezo mafupi juu ya maswali. Andika herufi unayoona ni sahihi katika kila swali au andika SI KWELI kwa swali unarofikiri halina usahihi na KWELI katika swali unalofikiri ni sahihi na kujaza sehemu iliyowazi au kutaja kinachotakiwa kutajwa.
1.Mwanachama yupi alitoa wazo la kuchapishwa t-shirts za PamoJah? A. Babukadja B. Dismas C. Michuzi Jr.
2. Taja majina mawili ya wana PamoJah waliopewa onyo kutokana na utovu wa nidhamu hapa kijijini.
3. Taja majina 15 ya wanachama wa PamoJah waliojiunga Baada ya Tarehe 23-Dec-2009.
4. A. Magere B. Mujydbubz C. Lucie wa Mama, D. Vadonde, E. George Rutenge mmoja wao ni wa kwanza kuvaa t-shirt ya PamoJah.
5. Chaoga, Mtoto Mzuri, Pascal, Ndekia, Michuzi Jr. Dismas ni wanachama wa PamoJah kwa sasa.
6. Taja jina la Muanzilishi wa FOTOBARAZA FONDATION.
7. Taja jina halisi la Mkuu wa Malavidavi ( Love Affairs)
8. Young alitembelewa na wana PamoJah 5 waliokwenda kumpa pole kutokana na msiba wa mama yake (YOUNG), taja majina yao.
9. Taja jina la msanii wa kiume aliyewahi kuonekana katika mchezo wa kuigiza akiwa amevaa T-shirt ya PamoJah katika kituo cha ITV.
10. Taja jina la msanii wa kike aliyewahi kuonekana amevaa t-shirt ya PamoJah katika mchezo wa kuigiza katika kituo cha ITV.
SHINDANO HILI LITAISHA SIKU YA ALHAMISI TAREHE 17-9-2009, SAA SITA MCHANA
KUJIBU MASWALI NI MARA MOJA TU, MSHIRIKI ATAKAYESHIRIKI ZAIDI YA MARA MOJA ATAKUWA AMEJITOA KATIKA SHINDANO HILI. ZAWADI KUTOLEWA NA MDHAMINI WA SHINDANO HILI, BWANA OSWALD JOHN AKYOO.
ZAWADI HAITABADIRISHWA KWA FEDHA.
PamoJah
na senksi so mach indidi!!!
Tags:
Shirikisha
-
▶ Jibu Hoja Hii